Watumishi wa umma wanaingia mwaka wa 6 wakiwa na mshahara ule ule uliopanda kwa mara ya mwisho mwezi July, 2015

Watumishi wa umma wanaingia mwaka wa 6 wakiwa na mshahara ule ule uliopanda kwa mara ya mwisho mwezi July, 2015

Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha...
Ndugu yangu kuwa na imani na wewe pekee ,kumwamini mtu mwingine yeyote ni kosa kubwa sana, hata pale unapoambiwa ni mchana toka ukahakikishe mwenyewe,kwani yaweza kuwa usiku,mwisho wake utaisia kuliwa na simba.
 
Bro, unajitahidi sana kuwasemea watumishi lakini njaa zao zinawafanya serikali iwatumie kama TP
Hahahaaaa huwa napenda sana nyie mnao jifanya hamtaki kuonewa wakati hata hapo ulipo usha onewa na kunyimwa haki zako kibao na hujafanya lolote .
 
Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha...
Ukweli mchungu;
  • Mishahara inaendana Na uwezo wa serikali
  • Kabla ya JPM serikali ilikuwa inakusanya sh 850 bilioni na wage bill ilikuwa wastani bilioni 600!
  • Matokeo yake ilishindwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati Na kutoa huduma bora Kama matibabu, elimu kwa watanzania wote.
  • Thamani ya pesa (inflation) liporomoka kwa kasi kuliko ongezeko dogo la mishahara
  • Seriakali ipo kwa ajili ya mamilioni yote ya watanzania Na siyo watumishi wa umma wasiofika milioni moja
  • Pamoja na kutopanda mishahara kakini thamani ya pesa imeongezeka sana, ambayo kiuhalisia ni sawa Na ongezeko la mishahara kuliko kipindi ambapo mishahara iliongezwa figuratively.
  • Ni akili kubwa kuongeza makusanyo Na kuwekeza kwanza kwa manufaa ya watanzania wote Na kukuza uchumi Na baadaye ukishatimiza malengo uliyojiwekea (of course ni ya muda mfupi au wa Kati) unaongeza mishahara ya hao watumishi.
  • Wakati huo huo unahakikisha unaongeza ufanisi wa utoaji huduma kama matibabu kwa watanzania wote
 
Ila pesa ya kujenga chato ipo. Sasa anajenga chuo cha mafunzo ya Serikali na uwanja mkubwa kuliko wote wa michezo Africa kwa gharama ya $400 millions.
Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha....
 
Ila pesa ya kujenga chato ipo. Sasa anajenga chuo cha mafunzo ya Serikali na uwanja mkubwa kuliko wote wa michezo Africa kwa gharama ya $400 millions.
Bwana yule hana roho ya utu.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Watumishi wa imma wa nchi hii ni bure kabisa, wengi wao wamejawa woga, ubinafsi na unafiki mno... Wanashindwa kuitambua nguvu kubwa walio nayo.
Lakini hiyo yote ni matokeo ya mfumo wetu wa elimu unaotumika "kuwapakaza" ujinga wahitimu badala ya kuwafuta.
 
Inapofikia mpaka binadamu wengine wanakuombea ufe ni lazima ujichunguze kwa kina unakosea wapi hadi uchukiwe kiasi hicho.
Yaani anajisahau mno. Anasahau kuwa hata yeye alikimbia ualimu kwasababu ya masilahi duni na akakimbilia kwenye siasa kutafuta masilahi bora. Binadamu ni wabinafsi mno!.
 
Tuliwalaumu na kuwalaani wakoloni kwa mambo mengi mojawapo ikiwa ni kutoa ujira mdogo kwa watu weusi na tukaamini tukipata uhuru, mambo haya yataisha...
Mishahara ya watumishi wangelipwa wabunge ingeshabadilika kitambo Ila kwasababu wao wanakula na kusaza hawana habari juu ya hilo.
 
Yaani anajisahau mno. Anasahau kuwa hata yeye alikimbia ualimu kwasababu ya masilahi duni na akakimbilia kwenye siasa kutafuta masilahi bora. Binadamu ni wabinafsi mno!.
Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
Tuendelee kumwombea Mungu ampende zaidi,ndio salama ya watumishi
 
Hakuna namna mtumishi wa sasa atafanya wala Viongozi wa vyama vyama vya wafanyakazi. Huwezi goma kazi kwa kuwa hata familia itakushangaa.

Maboss wote wenye sifa za kujaza fomu za Maadili wana masalary ya nguvu sana kiasi cha kusahau kabisa walio chini na wana tumia madinga ya Serikali.

Hahusiki na dalaldala huyu. Wao ndio wenye safari na marupurupu kama yote. Halafu anatokea Kiongozi anasema Walimu ni miongoni mwa watumishi wanalipwa mishahara mikubwa sana. Mungu anawaona.
 
Mh Rais aliahidi awamu yake hii ya pili ni ya neema kwa wafanyakazi, na mm naamini hivyo, tusubiri kuanzia July 2021.. Naamini ahadi ya Mh. JPM atatekeleza kwa watumishi mwaka wa 2021. Ukipita mwaka 2021, nitakosa imani na ahadi yake kabisa
 
Mh Rais aliahidi awamu yake hii ya pili ni ya neema kwa wafanyakazi, na mm naamini hivyo, tusubiri kuanzia July 2021.. Naamini ahadi ya Mh. JPM atatekeleza kwa watumishi mwaka wa 2021. Ukipata mwaka 2021, nitakosa imani na ahadi yake kabisa
Kwa pesa na UBINADAMU upi ?
 
Mh Rais aliahidi awamu yake hii ya pili ni ya neema kwa wafanyakazi, na mm naamini hivyo, tusubiri kuanzia July 2021.. Naamini ahadi ya Mh. JPM atatekeleza kwa watumishi mwaka wa 2021. Ukipata mwaka 2021, nitakosa imani na ahadi yake kabisa
Tuombe uzima tu ndugu.
 
Back
Top Bottom