Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Kuna mambo yanatia hasira sana.
Nashangaa wapo wachache wanayatetea.
Kabila la mtu linafanya kazi gani? Dini inasaidia nini ktk utendaji wa mtumishi?

Hawa watu wanawaza nini?!!
 
Tulia wewe kijana mdogo huna unalojua . Serikali ya nyerere ndio ilianzisha kuchukua taarifa za dini na kabila kwenye taarifa za kitaasisi hospitali, polisi, magereza hata kwenye fomu za kujiunga na utumishi wa umma
Ni Hospitali na Magereza tu tu ambako taarifa za dini zilikuwa zinachukuliwa kwa sababu iwapo mgonjwa akifa ijulikane maiti yake itafanywaje kwa misingi ya dini yake. Siyo kazini; mimi pia nilifanya kazi serikalini mwishoni mwa utawala wa Nyerere, Mwinyi na mwanzoni mwa utawala wa Mkapa; sikuwahi kuulizwa taarifa za dini yangu wala kabila langu !
 
Hapa nimeona wewe ndio mdini uliyepiyiliza.
Ni raisi gani aliwahi kutupa furaha na fursa watanzania? Mbona ni muongo hivi? Hayo unayosema Kama yangekua kweli Leo hii nchi isingekua maskini.
Swali; huko kwenu kwenye uislamu, mwanamke anaruhusiwa kuwa kiongozi?
 
Kwanini unashangaa hili, mbona mashuleni ni kitu cha kawaida miaka yote kuulizwa DINI yako na KABILA lako. Hii ipo siku zote mashuleni toka chekechea mpaka chuo kikuu. Nami kwa kweli siku zote nilikuwa najiuliza kwanini mwenendo huo uishie chuo kikuu na mavyuoni, katika ajira ni marufuku?

Nimefuatilia nchi nyingi (hata zilizoendelea UK, Amerika, Ufaransa n.k) kipengele cha dini kipo, kwanini kisiwepo TZ. Hivi tunaficha nini? Kwani huko makazini na mitaani hatujuani kuwa wewe ni dini hii na mii ni dini ile, kuna shida gani katika hilo au ikiwa katika makaratasi ndio tabu. Hivi tunaficha nini? Tusingejua dini za wabunge wetu hivi wangeapa kwa kutumia kitabu kipi, inamaanisha waliziandika dini zao katika fomu za ugombea. Tuache unafiki, kama tunataka transparency/uwazi mambo hayo ni lazima yawepo katika ngazi zote, kwa vile hiyo ndio identity yetu.

Kuna mashirika yanafahamika kuwa usipokuwa kabila fulani si rahisi kupata kazi. Niliwahi ambiwa kuwa TANROAD usihangaike kama si kabila fulani si rahisi kupata kazi, halikadhalika BIMA, BOT, n.k. Kama hii itawagusa poleni, ila ni njia sahihi kuelekea kwenye uwazi.
 
Jidanganye, sehemu nyingi suala la dini na kabila hujitokeza. Taasisi kubwa kabisa yenye kudai taarifa za dini ni elimu ya msingi na kuendelea, mgonjwa hospitali, ukikamatwa na polisi, mhimili wa bunge n.k.
 
Muongo mkubwa we!!!
 
Du hata kwenye sensa kipengele cha dini na kabila halipo,kwa kuamini Tanzania haina udini na ukabila, hata ukitaka kufanya tafiti mojawapo ya masharti ya kupitishwa kwa dodoso la utafiti ni kutokuweka kipengele cha dini na kabila.
Tafiti zipi? Kwenye medical kuna mashahidi wa yehova hao hata kuongezewa damu hawataki
 
Anajidanganya na anafikiri atafanikiwa kudanganya wengi. Bahati mbaya kaingia choo cha kike.

Hana point kabisa, kwani maswali hayo ya dini na kabila hujitokeza kila pahala taasisi inapotaka kujua identity yako.

Nchi iliundwa kinafiki nafiki tu na tunataka kuendelea na unafiki. Hapo hatujengi ni lazima tuwe wa wazi. Hivi unaona aibu kujulikana DINI yako na KABILA lako?
 
Magufuli hakua mdini, kwa kumbukumbu zangu zilivyo aliwatumbua na kuwaadhibu viongozi wengi Sana wa kikristo na wengine waliishia jela.
Labda sijui usemaje, Ila kwenye udini big NO
 
Use mkweli siku zingine! Magufuli alitumbua yeyote pamoja na wasukuma! Kama akina Charles Kitwanga waziri wa mambo ya ndani pamoja Charles Mlingwa mkuu wa mkoa wa mara! Msiwe waongo kwa chuki zenu za kikabila!
Akili yako haina akili. Kumtumbua kitwanga akawekwa nani vile.. usijitie umesahau Kiroboto.
Magufuli ndio mwalimu wa Samia wa haya yote. Tuendelee kushangilia ndio legacy yenyewe .
Hili ndio mnalonisikitisha Wapumbavu, mnashangilia wakiumizwa wengine na mnajiliza yakiwakuta.. pumbavu kabisa kabisa…

Sipendezwi na USHENZI wa Chui jike na sikupendezwa na UKICHAA wa Jiwe.
Sisi tunawakumbusha tu kuwa, muosha uwoshwa..! Mvumilie.
 
Huyu amekuja kuua nchi yetu
 
Kwa hiyo WAJANJA ni akina nani, na VILAZA akina nani? Kuna uhusiano wa wajanja/vilaza na MAKABILA/DINI.

Kama ni hivyo ngoja wajanja watoke mapangoni.
 
Reactions: Ame
Kama kutukanana na kudhalilishana kutakuwa kwa jinsi ya kabila huoni huo ni ukabila tayari? Hatuongozwi na rules za kabila wala dini yeyote sheria zetu siyo kama za Uganda au Kenya ambapo hayo mambo yalizingatiwa sisi yetu ni kutokana na katiba, acheni hayo mambo please!
 
Kwa maana kazini
Kwa vile kazini na mashuleni hawafi? Hapa umetoa mpya. Du, ni 2022! Ngoja Rais Samia awatoe mapangoni.
 
Mkuu sio kundi dogo, ni udini, element of Christianity, they want uchifu na uislamu na mambo maovu kama mimba mashuleni, wanawake kutawala dunia, kuweka nchi rehani kwa matajiri na mabeberu n.k ndio uelekeo unaoonekana kwa dots zilizopo,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…