Watumishi wa Umma waombwa na Hazina kuorodhesha Dini na Kabila zao. Rais Samia na Wasaidizi wako, haya yanafanyika kwa lengo gani?

Wazungu wana msemo mmoja usemao, "knowing your enemy is half winning the war", au kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi sana, "kumjua adui yako tu ni kushinda nusu ya vita yenyewe".

Hata kwenye mtihani, ukishalielewa swali tu tayari unakuwa umeshalifaulu nusu. Ndiyo maana Walimu huwa wanatusisitiza tusome swali tulielewe kabla ya kuanza kulifanya.

Sina cha kukujibu kwasababu hujanielewa ila umekimbilia ku-comment.
 
Reactions: Ame
Hivi ni vitu vya kawaida sana kuwepo kwenye CV.

Kwa kule Kigoma wakimbizi wengi wamejichanganya na wabongo na kujifanya wao ni watanzania na wapo wengi walioajiriwa kwenye shughuli mbalimbali.

Pengine record kama hizi ndio zitasaidia wengine waweze kupata kitambulisho cha Taifa.
 
Mbona Police unaulizwa kabila na Dini ? Acha Propoganda zako
 
Huu ni upumbavu na hatari kubwa!

Serikali inataka kujenga makanisa na misikiti? Serikali inataka kutengeneza taratibu za kufanya matambiko?

Mwalimu must be rolling in his grave!
Wasiokua na dini wanakomenti wapi?
Kama ni swala la kujua kabila na dini ya mtu si majina tu yanatosha kuonyesha hayo?
 
Baba yangu muasisi wa Taifa Mh. Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere . Ulijua madhara ya Udini na Ukabila ukavipinga na tukawa wamoja. Ule Umoja Baba haupo tena. Wanatugawa kwa Ukabila, Udini na Ukanda. Baba ninatamani ungefufuka uje ushangae na ukifa tena uombe usifufuke tena maana ni tishio kwa Yale mengi mazuri uliyojitolea kuyafanya kwa Taifa hili. Nimeandika kwa Uchungu Mkubwa mno. Tumekuwa wahanga ndani ya nchi yetu uliyotuachia yenye upendo na kupendana na kujaliana. Leo hii kuna mafisadi na wanaofisadiwa, Matajiri na Masikini wanaonyonywa mpaka tone la damu karibia wanakufa. Watu wako busy kugawana Ile keki Kwa kupeana madaraka na Ulaji. Mimi nisiyekuwa na God father ndiyo ninabaki kuchunwa mpaka mbavu zutavunjwa ili kundi Fulani lineemeke. Kama mtu mzima nimesikitika Sana.
 
Tena hata unapodahiliwa au kuomba mkopo wa chuo Kuna hivyo vipengele acheni Udini
 
Wasiokua na dini wanakomenti wapi?
Kama ni swala la kujua kabila na dini ya mtu si majina tu yanatosha kuonyesha hayo?
Mkuu wapo ambao ni wapagani. Ukweli nikiletewa hiyo fomu ningekuwa mtumishi wa Umma ningeandika sina dini. Ni huzuni kubwa mno. Upinzani uko wapi watoe press? Hili Jambo tusilifumbie macho kabisa. Leo ninaweka Uchama pembeni Kwa maslahi mapana. Ndiyo uzalendo na Umoja aliyoniachia hayati Baba wa Taifa kwa kunipa Elimu Bure na Huduma za Afya Bure. Hata maji ilikuwa ni Bure. Sipingi kuchangia Kwa kuwa Serikali Kwa sasa ilishabinafshisha vyanzo vyake vya mapato Ila nimekumbuka nilikotoka. Yaani kichwani kwangu sina dini wala Ukabila. Tena marafiki zangu wakubwa ni makabila tofauti na kabila langu na dini zote mpaka wapagani. Futeni hayo mambo ya dini na Ukabila haraka Sana.
 
Huyo ndiye haswa alisimamia Udini na Ukabila. Tunajua Mengi Ngoja tukae kimya. Vetting za enzi zile ndiyo ninayoyaona live sasa.
 
Umeliweka vizuri hili, sikuona huo uzuri wa Magufuli ambao watu wanausema hapa na pia siuoni huoni huo uzuri wa Samia watu wanausema hapa.
Nilichokiona Kuna watu wameamua kuwa wajinga na wapumbavu
 
jaza mpagani,
 
Mfanyakazi anaweza kufa kazini ghafla inabidi tujue dini yake ili tujue mwili wake utafanywaje
 
Hii haiko sawa
Tunakoelekea siko
Zoezi hili lisitishwe asap
 
Sasa hamuwezi amini, leo hii Hazina inaomba taarifa za watumishi (CV), na miongoni mwa taarifa wanazotakiwa kujaza hao watumishi ni:-
1. Kabila lako .....
2. Dini yako .......
Hii kitu huwa inafanywa polisi pia kama ukienda kushtaki au kushitakiwa
 
Mfanyakazi anaweza kufa kazini ghafla inabidi tujue dini yake ili tujue mwili wake utafanywaje
Unataka ushughulike na marehemu kama nani?
Mfanyakazi anapashwa kuweka contact information ya ndugu jamaa kama kuna jambo la dharura... hao ndio watajua imani ya Mtumishi
Hii dini kabila is nonsense
Vitambulisho vya Taifa ndio muhimu mengine hayawahusu (Uraia ndio muhimu) tumeajiri wageni wengi mno

Mtumishi aelimishwe namna ya kuandaa 'Will'
 
Waandishi wahoji kitu gani na hoja hakuna. Wananchi wanaulizwa dini na makabila yao sehemu nyingi sana za umma na hii haikuanza jana wala leo acheni ukuda
 
Kwa hiyo utafanyaje sasa! Maana keki ya taifa inaliwa na kila mtu saizi! Mwache mama afanye anavotaka! Maana nyinyi mlizoea kuiba saizi mambo yamebadilila sana! Vijana wenu wa kichaga wapo mtaani maisha yanawapiga kama kawa!
 
Juzi nimemsikia Mtoto wa Raisi wa Uganda ambaye ni mkuu wa maJeshi ya Uganda anasema nimeonhea na mjomba wangu Raisi P Kagame kuhusu mgogoro tumemaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…