BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 706
- 1,716
Kuna changamoto na adha kubwa tunapitia Watumishi wenye mahitaji maalum kwenye suala la uhamisho, tunapangiwa sehemu za kufanya kazi ambazo sio rafiki, hivyo inaathiri utendaji na inapotokea tunafuatilia uhamisho barua zinapokelewa Kama ushahidi TU hazifanyiwi kazi.
Mara nyingi tunapofuatilia tunaambiwa tujaze kwenye mfumo wa PEPMIS, mfumo ambao bado unachangamoto kubwa katika utendaji wake na nimekuwa nikiona hata baadhi ya Wanachama wa JF wakielezea hoja hiyo mara kadhaa.
Kwahyo tunaomba mamlaka zipokee barua ana kwa ana kwa Watumishi wenye mahitaji maalum hasa Walimu.
Nyongeza kwenye hilo pia tunashindwa kuelewa kuna namna nyingne yakupata uhamisho kwa Watumishi maana unakuta wengne pamoja na kuwa na sifa ya kuhama kama vile wenye mahitaji maalum hatupewi kibali cha kuhama lakini Watumishi wengine wanahama, ukifatilia utaambiwa bila konekisheni hutoboi.
Kero hii itatuliwe kwa uharaka ili Watumishi wenye mahitaji maalum tupate vibali vya kuhama ✍️✍️.
Sambamba na hilo watumishi wenye mahitaji maalum tupewe fursa ya mikopo yenye masharti nafuu, kama vile tupewe kipaumbele kwenye ile mikopo inayotoka Hazina kwa ajili ya Watumishi.
Serikali ipanue wigo pia kwa Watumishi wenye mahitaji maalum tupate mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri lengo ni kuepuka mikopo maarufu kama kausha damu✍️.
Naomba Serikali ilifanyie kazi suala hilo la mikopo kwa Watumishi wenye mahitaji maalum kuondokana na adha ya mikopo ya kausha damu ✍️.