Swali ni , je? Kwakuwa kuna wengine wamepata mshahara wa muundo mpya mwezi June,itakuwaje kwa hawa ambao walitakiwa kupata sambamba na hawa? Kwamba watapata na ya mwezi uliopita? Kwasababu hakuna sababu za msingi za kutowapandisha ikiwa tayari walikamilisha kila taarifa.
Kiukweli serikali inawadharau sana kundi fulani la watumishi.Wakati wanawajibika na kufanya kazi kwa mujibu ya miongozo na matakwa yake.Si sawa.
Tanzania inahitaji GEN Z wakali zaidi ya Kenya.
Watumishi mishahara yao ni ileile kiduchu pamoja na kupanda kwa gharama za maisha.
Kama kuna watumishi ambao walikwama kwenye cheo kimoja kwa miaka saba hadi kumi, kuna shida gani kuwapandisha walau madaraja mawili kwa mserereko.
Kwa sasa kigingi walicholeta kuwakandamiza watumishi ni PEPMIS, na vyama vya wafanyakazi vipo vinaona ni sawa tu.
Hawa watu wakishapata migao yao kwenye dili za bandari na mbuga wanajiona wao ndo wanastahili kuwa na maisha bora kuliko watumishi wa kawaida na watanzania wengine.