DOKEZO Watumishi wa Umma zaidi ya 80% hawajapandishwa madaraja ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 unaoisha. Hii ni dhulma kubwa

DOKEZO Watumishi wa Umma zaidi ya 80% hawajapandishwa madaraja ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 unaoisha. Hii ni dhulma kubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Swali ni , je? Kwakuwa kuna wengine wamepata mshahara wa muundo mpya mwezi June,itakuwaje kwa hawa ambao walitakiwa kupata sambamba na hawa? Kwamba watapata na ya mwezi uliopita? Kwasababu hakuna sababu za msingi za kutowapandisha ikiwa tayari walikamilisha kila taarifa.

Kiukweli serikali inawadharau sana kundi fulani la watumishi.Wakati wanawajibika na kufanya kazi kwa mujibu ya miongozo na matakwa yake.Si sawa.
Tanzania inahitaji GEN Z wakali zaidi ya Kenya.
 
WANAMTUMA MSONDE KU SPIN HILO SWALA KWA VIKAO VYA KISHENZI KWA WALIMU NCHINI!!

HALAFU WANATUOMBA KURA TUMPITISHE SAMIAH KWA KISHINDO!!

WATAMPITISHA WANAJESHI NA POLICE HAO NDIO KAZI YAO NCHINI!!​
Watumishi mishahara yao ni ileile kiduchu pamoja na kupanda kwa gharama za maisha.

Kama kuna watumishi ambao walikwama kwenye cheo kimoja kwa miaka saba hadi kumi, kuna shida gani kuwapandisha walau madaraja mawili kwa mserereko.

Kwa sasa kigingi walicholeta kuwakandamiza watumishi ni PEPMIS, na vyama vya wafanyakazi vipo vinaona ni sawa tu.

Hawa watu wakishapata migao yao kwenye dili za bandari na mbuga wanajiona wao ndo wanastahili kuwa na maisha bora kuliko watumishi wa kawaida na watanzania wengine.​
 
Tuwe na subraaa jamani mama samia anawawazia mambo mema.. ngoja ma DC wamaliziwe kugawiwaa magari yao mapya.
 
Back
Top Bottom