A
Anonymous
Guest
Kuna Watumishi wa Wizara ya Maji wanaolalamikia kutokudhibitishwa kazini licha ya kuwa wamekaribia kutimiza miaka miwili tangu waajiriwe.
Watumishi hao wanasema hawaelewi sababu ya kucheleweshewa kuthibitishwa kazini baada ya kutimiza masharti ya kiutumishi yanayohitajika kwa hatua hiyo. Wanaeleza kuwa wameajiriwa tangu Agosti 2024, lakini hadi sasa hawajathibitishwa kazini wala kupewa maelezo ya kina kuhusu chanzo cha ucheleweshaji huo.
Kwa mujibu wa watumishi hao, kila wanapoulizia suala hilo huambiwa wasubiri na kwamba watapatiwa taarifa baadaye, lakini hadi sasa hawajapata ufafanuzi wa kutosha kuhusu lini mchakato huo utakamilika.