RESOLVED Watumishi wapya wa Sikonge tumelipwa fedha za kujikimu, shukrani sana

RESOLVED Watumishi wapya wa Sikonge tumelipwa fedha za kujikimu, shukrani sana

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Imefanyiwa kazi au kupatiwa ufumbuzi na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Sisi ni watumishi wapya wa Idara ya Afya tulioajiriwa mwaka 2025/2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora. Awali tuliwasilisha malalamiko yetu kupitia JamiiForums.com kuhusu kutolipwa fedha zetu za kujikimu baada ya kuripoti vituoni.

Hoja ya awali ~ Watumishi wapya wa Idara ya Afya katika Halmashauri ya Sikonge hatujalipwa fedha za kujikimu

Tunapenda kutoa shukrani kwa mamlaka husika baada ya kufuatilia suala hilo, kwani hatimaye tumelipwa fedha hizo ambazo tulikuwa tukizidai.

Tunathamini hatua iliyochukuliwa na tunaiomba Serikali kuendelea kuhakikisha watumishi wapya wanapata stahiki zao kwa wakati ili kuwawezesha kuanza majukumu yao kwa ufanisi na moyo wa kufanya kazi. Asante kwa JamiiForums.com kwa kutupa nafasi ya kufikisha sauti yetu.
 
Back
Top Bottom