Watumishi wasiozingatia Maadili Kuchunguzwa

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Utumishi wa Umma nchini kufuatilia kwa karibu Halmashauri zote nchini na kubainisha Halmashauri ambazo hazizingatii maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma ili waweze kupunguza mienendo ya watumishi hao ya kutokuzingatia maadili.

Wana-jamvi mnalionaje hili, litakuwa na msaada wowote kwa maendeleo ya Taifa letu?
Ethics.jpeg
 
Ni jambo jema. Waanze wao serikali kuu kudhibiti baadhi ya mambo yanayozuia kasi ya utendaji kwa kujilimbikizia mali, na kusababisha pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.

Hivi hawaoni aibu kuwapa masharti magumu watumishi wenye hali duni ilihali wao wakijiagizia magari mapya kila wakati?

Kama kuna mmomonyoko wa maadili wajaribu kujua chanzo chake ili kusaidia kuliko kuzidi kuweka sheria kandamizi
 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Utumishi wa Umma nchini kufuatilia kwa karibu Halmashauri zote nchini na kubainisha Halmashauri ambazo hazizingatii maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma
Anayejua mafanikio aliyotupa Jenista tangu apate uwaziri atuorodheshee hapa
 
Hapo utashangaa itaundwa kamati ya upigaji hela za wavuja jasho ya kuzunguka nchi nzima, ili kufanya huo uchunguzi.
 
Ni jambo jema. Waanze wao serikali kuu kudhibiti baadhi ya mambo yanayozuia kasi ya utendaji kwa kujilimbikizia mali, na kusababisha pengo kubwa kati ya walionacho na wasionacho.

Hivi hawaoni aibu kuwapa masharti magumu watumishi wenye hali duni ilihali wao wakijiagizia magari mapya kila wakati?

Kama kuna mmomonyoko wa maadili wajaribu kujua chanzo chake ili kusaidia kuliko kuzidi kuweka sheria kandamizi
Naunga mkono hoja
 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Utumishi wa Umma nchini kufuatilia kwa karibu Halmashauri zote nchini na kubainisha Halmashauri ambazo hazizingatii maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma ili waweze kupunguza mienendo ya watumishi hao ya kutokuzingatia maadili.

Wana-jamvi mnalionaje hili, litakuwa na msaada wowote kwa maendeleo ya Taifa letu?View attachment 2524216
serikali ya kutoa amri kila siku. inaonekana hata wakuu wa mikoa na wilaya hasa maDED hawana kazi nyingine isipokuwa kusubiri matamko na amri za mawaziri...it is too much. As if hakuna mwongozo wa utendaji kazi
 
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama ameiagiza Tume ya Utumishi wa Umma nchini kufuatilia kwa karibu Halmashauri zote nchini na kubainisha Halmashauri ambazo hazizingatii maadili ya utendaji kazi katika utumishi wa umma ili waweze kupunguza mienendo ya watumishi hao ya kutokuzingatia maadili.

Wana-jamvi mnalionaje hili, litakuwa na msaada wowote kwa maendeleo ya Taifa letu?View attachment 2524216
Kwahyo watu wa Tamisemi hawatakiwi kulamba asali?
 
Waanze na vijana wa Magufuli, Magu hakuficha hela Uswisi peke yake. Kuna watu walimsaidia.
 
Back
Top Bottom