tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Ukienda Wizara ya Afya, utakuta kuna watumishi kedekede, wanaosimamia jambo ambalo hawajawahi lifanya. Kuna wafamasia, ambao hawajawahi toa hata kidonge kimoja kwa mgonjwa, kuna madaktari ambao hata ndugu yake akiumwa Typhoid atapiga simu kwa daktari mzoefu hospitalini amtajie dawa nzuri. Kuna wauguzi ambao hawajui adha ya kugeuza mgonjwa maeneo kusikokuwa na magodoro maalumu. Hivi inakuwaje mtu hana uzoefu wa kutibu anasimamia sera zinazoendana na matibabu?
Hawa watu hawajui hata vifaa gani vinatakiwa katika taasisi zetu. Elimu waliyonayo ni ile waliyoipata shule. Hawana uzoefu zaidi ya kufanya utarajali tu (internship). Wanahusika kutengeneza miongozo ya magonjwa mbalimbali, lakini hawajawahi tibu hata mgonjwa mmoja. Kila wakati wanaenda kufanya mentorship na supportive supervision ya vitu wasivyovifahamu.
Watu hawa ndio wanatuangusha, kila siku wanashinda wakizunguka huku na huko na computer. Mtu kama huyu atajuaje changamoto zilizopo katika taasisi za afya? Changamoto zote zinapaswa uziishi.
Wengine wanaofanana na hawa ni wale ambao, alipofika tu Wilayani wakapewa ama uganga ufawidhi au uganga mkuu wa wilaya, na sasa ni makatibu wakuu au wakurugenzi kwenye wizara nyeti, hawajui adha za kuwa mdogo, hawajui changamoto za chini. Ni style ya Dr. Gwajima.
Tufuate mfumo wa Japan, unaanza ngazi ya kwanza kufika ngazi ya juu.