GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
CAG mstaafu, Prof. Assad aliposema asilimia sitini ya watumishi wa uma hawana uwezo, Serikali ilijitokeza haraka sana kukana hilo.
Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba aliposema kuwa asilimia tisini ya wasomi wetu wanajua tu kusoma na kuandika, watu wengi walimkejeli.
Lakini kwa hali ya mambo ilivyo nchini, nani anaweza tena kuendelea kukanusha hayo madai?
Kama siyo ukilaza, uwizi, na uvivu wao, reli ya SGR ingekuwa haijakamilika mpaka sasa? Magufuli angekuwepo hali ingekuwa ilivyo sasa?
Kama siyo ubinafsi wao, mgao wa umeme ungetesa kwa muda mrefu kama ilivyotukia? Siyo kwamba huo mgawo ulikuwa wa mchongo kwa manufaa ya wachache?
Nimemwona Makonda akiwahoji baadhi ya watumishi mkoani Arusha! Utawaonea wengine huruma. Hawayajui majukumu yao. Ni kama wapo wapo tu.
Fikiria kwa mfano Afisa Biashara mmoja ambaye yeye anajua tu kukusanya ushuru kwenye minada ya Kijiji lakini hajui asilimia ya mapato yanayotakiwa kurudishwa kwenye hicho kijiji. Halafu eti huyo ni mkuu wa idara! Aibu iliyoje!
Arusha walipatiwa bilioni thelathini na Saba katika mwaka wa fedha 2023/2024, lakini ni bilioni kumi na saba tu ndizo zimetumika. Bilioni ishirini zitarejeshwa hazina. Kutafuta hela hawajui na hata kutumia walizopewa hawawezi. Huo ni ukilaza na uvivu uliokithiri.
Kuna mahali wilayani Longido walikuwa wanakusanya mapato ya shilingi milioni kumi na tatu kwa mwezi au wiki, (sikumbuki vizuri), lakini baada ya mianya ya upigaji kuthibitiwa, mapato yakaongezeka kutoka milioni kumi na tatu hadi mia moja ishirini kwa wiki/mwezi. Ona wasivyokuwa na huruma! Walikuwa wanaiba zaidi ya milioni mia moja kwa wiki/mwezi huku Serikali ikiambulia milioni kumi na tatu pekee.
Hiyo ni Arusha tu! Sijui kwenye mikoa mingine kukoje. Lakini inasemekana huo ni mtindo uliozoeleka maeneo yote.
Kama ndivyo, ni dhahiri kuwa ofisi za uma zimegeuka vichaka vya wezi, vilaza, wavivu, wenye viburi n.k.
Najua siyo wote, lakini asilimia nyingi ndivyo walivyo. Labda, ni kwa sababu wengi wao wamepata hizo nafasi kwa "connection", ama wamezinunua au wamewekwa na ndugu zao. Ndiyo maana hata baadhi ya madereva wa magari ya uma huonesha kiburi wawapo barabarani. Kwa sababu tu anaendesha gari la Serikali hudiriki hata kuvunja Sheria za usalama barabarani kwa kuwa anajua kuwa hatachukuliwa hatua kama wengine.
Naamini, kama siyo hao watu: vilaza, wezi, wavivu, wenye viburi, n.k. kujazana kwenye ofisi za uma, nchi yetu isingehitaji kwenda kuomba misaada nchi za nje kama South Korea. Lakini sasa itafanyaje ikiwa hela inayotafunwa na kuchezewa ni nyingi kuliko inayoingia kwenye matumizi sahihi?
Laiti lingepita fagio la kusafisha ofisi za uma dhidi ya vilaza, wezi, wavivu na wenye viburi, nchi yetu ingesonga mbele kwa maendeleo.
Kama aina hiyo ya watumishi wataendelea kuwepo kwenye hizo ofisi, kasi ya maendeleo ya nchi yetu itaendelea kuwa ya kusuasua. Labda kama wataamua kubadilika.
Swali ni kwamba watabadilika?