Kuna baadhi ya vifungu kwenye Bible uki connect dott unapata picha tofauti kabisa kuhusu Dini.
Wakati wa Biashara za watumwa, Watumwa walivyo kuwa wanafika kule hawakuruhusiwa kujifunza kitu tofauti na Dini.
Na Dini ndo kitu cha kwanza walicho kuwa wanafundihswa walivyo fika kule, na kuna baadhi ya vifungu walikuwa wanasisitiziwa zaidi kusoma kama Waefeso 6:5.
Unazani Wamiliki wa watumwa waliwapenda sana Watumwa na wakataka waende mbinguni ndo maana wakawa kitu cha kwanza ni kufundishwa Dini na hata kubatizwa na kupewa majina ya Kidini?
Kuna meli moja iliyobeba watumwa toka Afrika ya Magharibi kwenda Amerika iliitwa
"Jesus" japokuwa hii haikumaanisha kwamba mmiliki ni muumini mzuri wa Ukristo lakini elewa slave masters walitumia sana dini ili kuweza kuwa-control watumwa. Sina uhakika na Waefeso 6:5 lakini kuhusu vifungu vya Bibilia kutumika wakati huo si jambo geni kabisa kama kweli wewe ni mfatiliaji wa historia.
Mwanzoni mwa karne ya kumi na tisa, watumwa wengi walikuwa Wakristo. Wapo waliokubali Ukkristo kwa hiari, wakati wengine walikuwa wamefanya hivyo kwa kulazimishwa na mabwana zao. Slave masters waliona Ukristo kama njia muhimu ya kudhibiti jamii. Kwa kusisitiza sifa za
Kikristo za
upole, uvumilivu, na uadilifu, walitumaini kuhamasisha watumwa wao kuwa wafanyakazi wanyenyekevu.
Ingawa walitaka watumwa wao wahudhurie ibada za Kikristo lakini hawakutaka waende peke yao. Makanisa ya watumwa yaliyokuwa na uhuru yalipigwa marufuku na kuamriwa kuabudu chini ya
usimamizi mkali wa wazungu. Walihofia kwamba kama wangewaacha waabudu wenyewe watumwa wao
wangefasiri mafundisho ya Yesu Kristo kuwa yanapendelea usawa. Hii pia ni moja ya sababu kuu kwa nini wamiliki wengi wa watumwa hawakutaka watumwa wao wajifunze kusoma.....
ref. University of Rochester - Frederick Douglass Project, DOCUMENT PACKET: REPRESENTING SLAVERY /
The Narrative of William W. Brown, a fugitive slave by Brown, W.W. (1848).
Ndugu elewa utaratibu huu haukuwa kwa wazungu tu hata waarabu walipokuja Afrika na kuanza biashara ya utumwa walileta dini pia huku wakiendelea kututesa.