GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Nilikuwa nikiwachukulia viongozi wa dini kama watu waliofilisika mawazo wanapoongelea masuala ya tabia nchi. Sikuona sababu ya wao kuongelea masuala hayo wakati kuna wataalam wanaohusika nayo.
Ni mpaka nilipoelewa Andiko la Mwanzo 7: 1 - 5 kwa namna nyingine ndipo "nilipowaelewa"
Duniani kote, kuna taasisi mbalimbali na watu binafsi wanaofanya jitihada za kuyatunza mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vya baadaye. Wanaofanya hayo wanafanya kazi ya Mungu hata kama hawalijui hilo wala kuamini katika Mungu.
Biblia inaonesha kuwa Mungu ndiye Muhifadhi wa kwanza. Mwanzo 7:1- 5 inathibitisha.
Imeandikwa, "BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina... Katika wanyama wote walio safi ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama wasio safi wawili wawili wawili, mume na mke. Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ili kuhifadhi hai mbegu juu ya uso wa nchi yote... Nuhu akafanya kama vile BWANA alivyomwamuru"
Andiko hilo linaonesha kuwa hakutaka uumbaji wake upotee, iwe ni mimea au wanyama.
Nashawishika kuamini kuwa Mungu anapendezwa na watu wanaojitajidi kuyatunza mazingira ili kuwezesha viumbe vyake kuishi "comfortably ". Wanaofanya hivyo wanamtumikia Mungu bila wao kujua.
Kwa uelewa huo, nimeacha kuwashangaa Wazungu waliojenga hospitali za kisasa huko kwao kwa ajili ya wanyama wao.
Hili ni sahihi kwa sababu Mungu hataki uuambaji Wake uteseke.
Mungu anathamini viumbe vyake vyote: miti, maua, mimea mbalimbali, chura, mijusi, mamba, Kobe, Faru, Tembo, Simba, Chui, nyani, kima, vinyonga, mchwa, n.k.
Kama wewe ni miongoni mwa watunza mazingira, hata kama unafanya peke yako, ujue unafanya kazi ya Mungu. Endelea kufanya hivyo.