Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
Kardinal Pengo ana haki zote kuhoji ni wapi upepelezi wa mauaji na kupigwa risasi kwa mapadri kulikofikia. Kardinal Pengo akiwa kiongozi mkuu wa mapadri na waumi wake ana haki za kuhakikisha ulinzi wa kiroho na kimwili wa anaowathamini na kuwaongoza unazingatiwa. Utakuwa kiongozi wa ajabu sana unaposahau unaowaongoza hasa wakati wa mahitaji.
Majibu ya polisi ni ya kihuni na yasio na busara hasa pale ambapo tatizo lilipo ni la ukweli na linachanganya kila mmoja.
Vitisho vya mauji utekwaji nyara, mateso nk vimekuwa vikitokea huku polisi, usalama wa taifa nk wakila mishahara ya kodi zetu na kujenga kiburi.
Akiwa maezungukwa na polisi walisheheni silaha, Mwangosi aliuwawa kikatili mikononi mwa polisi na polisi wenyewe. Akiwa amezungukwa na usalama wa taifa raisi mstaafu Ali Hasan mwinyi alizabwa kibao, sheikh wa Zanzibar alimwagiwa tindikali. mwiningine alichomwa Kisu akafa. Polisi ikiwa inajua Mchungaji Buserere alichinjwa kama Kuku. Akiwa natetea haki za Madaktari Ulimboka alitekwa akatolewa meno na kucha bila Ganzi. Akiwa ofisini kwake alimwagiwa ----- na kumbadili ngozi- Mwakyembe. Akiwa kwenye gari tairi lilichomoka -Raisi jakaya Kikwete. Akiwa ikulu Taa za benz ziliibwa. Sioni wapi ni salama.
Visa vya kukosekana walinzi wa nchi ni vingi sana. Hii inadhihirisha kabisa vitengo vyeti vyote vya usalama vimeshindwa kazi au wakurugenzio wao na mkubwa wao wamekuwa wazembe wa kutokufanyiwa taarifa kazi. Kila nikiongea na wakusanya na watafiti wa kijasusi wanajitetea kuwa taarifa zote wakubwa wanazo kazi yao inakuwa imeishia hapo wanasubiri amri.
Yote hapo juu ni baadhi ya matukio yaliyokosa majibu isipokuwa moja tu la Kuuwa kinyama Kamanda wa Polisi wa Mwanza uchunguzi uliwezekana na wahalifu wakakamatwa.
Tatizo la hisia za udini limekomaa sana na ni hatari kwa ustawi na ukuaji wa jamii yetu. Ile hali ya kuheshimiana na kuvumiliana kidini na kiimani imepotea kabisa. Baada ya dini nayo kuingia kwenye soko huria kweli imekuwa huria. Wahubiri hawaheshimu tena sheria za nchi wala hawahubiri dini kutokana na vitabu wanavyotabanisha kuviabudu. Majukwaa ya dini yamekuwa majukwaa ya kushambuliana kama sio dini moja na nyingine basi sehemu ya Jamhuri na nyingine. Hii ni hatari sana.
Majukwaa ya dini na viongozi wao wanatamaka wazi kuuwa na kudhuru waumini wa dini nyingine bila woga na kificho. Walinda usalama wapo wanasikia na wanaona. Haijaishia hapo tayari masheikh wamekufa , wachungaji wamekufa na mapadri wamekufa tena wote wameuwawa ama kwa risasi, kuchinjwa au kuchomwa visu.
Chuki hii imepandikizwa mpaka kuanza kuchukia nyumba za ibada na kuzichoma moto na hakuna sheria wa karipio linalotolewa zaidi ya kauli za mlipuko kama kawa.
Kwa yeyote anayeendekeza udini kwenye siasa kwa sababu zozote zile ajue tu hakuna nchi yeyote duniani yenye amani hivi leo amabyo viongozi wake wamekumbatia ubaguzi wa aina yeyote ile. Makaburu pamaoja na fedha zao walishwa, Wamarekani pamoja na wingi wao wa wazungu walishindwa. Sadam hussein alishindwa pamoja na wingi wa dini moja. Ulaya wameshindwa. Hata Vatican iliruhusu msikiti ujengwe. Huu ndio udugu wa kweli na undungu unaosemwa kwenye vitabu vyote vitakatifu.
Serikali ya Rais jakaya Mrisho Kikwete, inatakiwa iwe wazi kulinda, kuitetea na kuitunza katiba ambayo kwayo wote waliapa kuilinda. Dini zote lazima zifanye kazi zake zikizingatia katiba ya nchi. uchochezi usingojewe mpaka afe padri, Imam, mchungaji ndio serikali iamke. majibu ya Kejeli yanayotolewa na Polisi yanatuuzi wote.
Kusema kweli siku ikitokea kanisa likachomwa na msikiti ukachomwa moto utawaka kweli kweli. Na hii haiko mbali kama viongozi hawatakuwa makini. hakuna ugomvi mbaya kama wa kidini. Wahanga wa kwanza ni Watanzania masikini.
Kauli ya Maaskofu ya kukosa imani na utawala uliopo madarakani sio kauli ya kupuuza hata kidogo. Kwasasa ni kauli ambayo kila Muumini wa kikristu anaamini kabisa serikali ipo kwa ajili ya kumtesa na kuachwa bila mtetezi. Kauli ya waislam ya mfumo kristo nayo imezaa uharakati wa kudai haki kutoka kwa wakristu ambayo wakristu wanashangaa ni mfumo gani wanao. Kauli mbiu hizi sio za kuziacha na sasa nasikia wakristu nao wanasema mfumo islam.
Bila kuzikumbusha taasisi za dini zifanye kazi ya kuhubiri dini na kuachana na siasa tutaangamia. Bila sheria kuhakikisha inalinda imani ya kila mmoja bila kuingiliwa na dini nyingine tutaangamia. Bila serikali kuhakikisha inakomesha kabisa kashfa za kidini bila kujali nani anakashfu tutaangamia. Bila serikali kukomesha kabisa madhabahu na mihadhara ya dini kuwa majukwaa ya kisiasa tutaangamia.
Sielewe kwanini kiongozi atoae kauli za kwenda kuuwa halafu aachwe huru. Sielewi kwa nini kiongozi au mhubiri kwenye mahubiri yake yote ni kutaja dini nyingine kana kwamba kitabu chake kililetwa kwa ajili ya kupambana na dini husika. Sielewi kwanini Katiba inayotamka wazi binadamu wote ni sawa na kila raia ana haki ya kufiuata dini yeyote ilimradi havunji sheria kwanini atukanwe na abugudhiwe na katiba isimlende.
Maaskofu wametoa kauli ambayo ikiletewa dharau itazaa madhara makubwa sana. Siamini kama ajira za leo ziko kutokana na jina lako zaidi ya uwezo wako. Naishi na Watanzania wenzangu na hatujuani kwa dini, kabila, wala rangi bali utanzania wetu. Huu umasikini wa akili ni mbaya sana na unataka kulingamiza Taifa.
Ni wajibu wa serikali kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila raia anahaki ya kuabudu apendavyo bila kuingiliwa na sheria yeyote ile inayoonyesha ubaguzi.
Anayetaka kuchinja kwa kunyonga ruksa, kwa kukata ruksa. Mla panya ruksa, mla kobe ruksa.
Swala la uchinja lisiwe swala la serikali, hii iwe fursa kwa wafanyabiashara kwa kutambua wateja wao. Hili swala sidhani kama ni kubwa isipokuwa serikali ndiyo chanzo kikubwa. Kila raia anahaki ya kuchinja mnyama salama aliyekaguliwa. katiba haisemi nani achinje wapi na saa ngapi.
Tumeheshimiana sana, hata leo hapa kijijini kwetu bado naoana heshima ya enzi na enzi bado ipo. Ila favour ikibadilishwa sheria ndio balaa linaanza. hakuna raia namba moja wala mbili. Na kila dini ni bora kwa muumini husika.
Polisi acheni majibu mepesi kwa kuchezea imani za watu.
Chief Mkwawa
Tanganyika na Zanzibar ilikuwa na amani bila dini. Dini ni ujio wa wakoloni na waarabu. Dini za mababu zetu zilitufundisha upendo na kuheshimiana. Dini mpya zinatufundisha kuchinjana na kutukanana. Tusome upya hivi vitabu vya wageni. Vikitushinda turudi kwenye mapango yetu.