Wauaji sio kondoo maneno ya kashfa kutoka kwa walinzi wa mali zetu na raia-polisi

Wauaji sio kondoo maneno ya kashfa kutoka kwa walinzi wa mali zetu na raia-polisi

Mkwawa

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2011
Posts
1,334
Reaction score
1,466
Kardinal Pengo ana haki zote kuhoji ni wapi upepelezi wa mauaji na kupigwa risasi kwa mapadri kulikofikia. Kardinal Pengo akiwa kiongozi mkuu wa mapadri na waumi wake ana haki za kuhakikisha ulinzi wa kiroho na kimwili wa anaowathamini na kuwaongoza unazingatiwa. Utakuwa kiongozi wa ajabu sana unaposahau unaowaongoza hasa wakati wa mahitaji.

Majibu ya polisi ni ya kihuni na yasio na busara hasa pale ambapo tatizo lilipo ni la ukweli na linachanganya kila mmoja.
Vitisho vya mauji utekwaji nyara, mateso nk vimekuwa vikitokea huku polisi, usalama wa taifa nk wakila mishahara ya kodi zetu na kujenga kiburi.

Akiwa maezungukwa na polisi walisheheni silaha, Mwangosi aliuwawa kikatili mikononi mwa polisi na polisi wenyewe. Akiwa amezungukwa na usalama wa taifa raisi mstaafu Ali Hasan mwinyi alizabwa kibao, sheikh wa Zanzibar alimwagiwa tindikali. mwiningine alichomwa Kisu akafa. Polisi ikiwa inajua Mchungaji Buserere alichinjwa kama Kuku. Akiwa natetea haki za Madaktari Ulimboka alitekwa akatolewa meno na kucha bila Ganzi. Akiwa ofisini kwake alimwagiwa ----- na kumbadili ngozi- Mwakyembe. Akiwa kwenye gari tairi lilichomoka -Raisi jakaya Kikwete. Akiwa ikulu Taa za benz ziliibwa. Sioni wapi ni salama.

Visa vya kukosekana walinzi wa nchi ni vingi sana. Hii inadhihirisha kabisa vitengo vyeti vyote vya usalama vimeshindwa kazi au wakurugenzio wao na mkubwa wao wamekuwa wazembe wa kutokufanyiwa taarifa kazi. Kila nikiongea na wakusanya na watafiti wa kijasusi wanajitetea kuwa taarifa zote wakubwa wanazo kazi yao inakuwa imeishia hapo wanasubiri amri.

Yote hapo juu ni baadhi ya matukio yaliyokosa majibu isipokuwa moja tu la Kuuwa kinyama Kamanda wa Polisi wa Mwanza uchunguzi uliwezekana na wahalifu wakakamatwa.

Tatizo la hisia za udini limekomaa sana na ni hatari kwa ustawi na ukuaji wa jamii yetu. Ile hali ya kuheshimiana na kuvumiliana kidini na kiimani imepotea kabisa. Baada ya dini nayo kuingia kwenye soko huria kweli imekuwa huria. Wahubiri hawaheshimu tena sheria za nchi wala hawahubiri dini kutokana na vitabu wanavyotabanisha kuviabudu. Majukwaa ya dini yamekuwa majukwaa ya kushambuliana kama sio dini moja na nyingine basi sehemu ya Jamhuri na nyingine. Hii ni hatari sana.

Majukwaa ya dini na viongozi wao wanatamaka wazi kuuwa na kudhuru waumini wa dini nyingine bila woga na kificho. Walinda usalama wapo wanasikia na wanaona. Haijaishia hapo tayari masheikh wamekufa , wachungaji wamekufa na mapadri wamekufa tena wote wameuwawa ama kwa risasi, kuchinjwa au kuchomwa visu.

Chuki hii imepandikizwa mpaka kuanza kuchukia nyumba za ibada na kuzichoma moto na hakuna sheria wa karipio linalotolewa zaidi ya kauli za mlipuko kama kawa.

Kwa yeyote anayeendekeza udini kwenye siasa kwa sababu zozote zile ajue tu hakuna nchi yeyote duniani yenye amani hivi leo amabyo viongozi wake wamekumbatia ubaguzi wa aina yeyote ile. Makaburu pamaoja na fedha zao walishwa, Wamarekani pamoja na wingi wao wa wazungu walishindwa. Sadam hussein alishindwa pamoja na wingi wa dini moja. Ulaya wameshindwa. Hata Vatican iliruhusu msikiti ujengwe. Huu ndio udugu wa kweli na undungu unaosemwa kwenye vitabu vyote vitakatifu.

Serikali ya Rais jakaya Mrisho Kikwete, inatakiwa iwe wazi kulinda, kuitetea na kuitunza katiba ambayo kwayo wote waliapa kuilinda. Dini zote lazima zifanye kazi zake zikizingatia katiba ya nchi. uchochezi usingojewe mpaka afe padri, Imam, mchungaji ndio serikali iamke. majibu ya Kejeli yanayotolewa na Polisi yanatuuzi wote.

Kusema kweli siku ikitokea kanisa likachomwa na msikiti ukachomwa moto utawaka kweli kweli. Na hii haiko mbali kama viongozi hawatakuwa makini. hakuna ugomvi mbaya kama wa kidini. Wahanga wa kwanza ni Watanzania masikini.

Kauli ya Maaskofu ya kukosa imani na utawala uliopo madarakani sio kauli ya kupuuza hata kidogo. Kwasasa ni kauli ambayo kila Muumini wa kikristu anaamini kabisa serikali ipo kwa ajili ya kumtesa na kuachwa bila mtetezi. Kauli ya waislam ya mfumo kristo nayo imezaa uharakati wa kudai haki kutoka kwa wakristu ambayo wakristu wanashangaa ni mfumo gani wanao. Kauli mbiu hizi sio za kuziacha na sasa nasikia wakristu nao wanasema mfumo islam.

Bila kuzikumbusha taasisi za dini zifanye kazi ya kuhubiri dini na kuachana na siasa tutaangamia. Bila sheria kuhakikisha inalinda imani ya kila mmoja bila kuingiliwa na dini nyingine tutaangamia. Bila serikali kuhakikisha inakomesha kabisa kashfa za kidini bila kujali nani anakashfu tutaangamia. Bila serikali kukomesha kabisa madhabahu na mihadhara ya dini kuwa majukwaa ya kisiasa tutaangamia.

Sielewe kwanini kiongozi atoae kauli za kwenda kuuwa halafu aachwe huru. Sielewi kwa nini kiongozi au mhubiri kwenye mahubiri yake yote ni kutaja dini nyingine kana kwamba kitabu chake kililetwa kwa ajili ya kupambana na dini husika. Sielewi kwanini Katiba inayotamka wazi binadamu wote ni sawa na kila raia ana haki ya kufiuata dini yeyote ilimradi havunji sheria kwanini atukanwe na abugudhiwe na katiba isimlende.

Maaskofu wametoa kauli ambayo ikiletewa dharau itazaa madhara makubwa sana. Siamini kama ajira za leo ziko kutokana na jina lako zaidi ya uwezo wako. Naishi na Watanzania wenzangu na hatujuani kwa dini, kabila, wala rangi bali utanzania wetu. Huu umasikini wa akili ni mbaya sana na unataka kulingamiza Taifa.

Ni wajibu wa serikali kuhakikisha ulinzi wa raia na mali zao. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kila raia anahaki ya kuabudu apendavyo bila kuingiliwa na sheria yeyote ile inayoonyesha ubaguzi.

Anayetaka kuchinja kwa kunyonga ruksa, kwa kukata ruksa. Mla panya ruksa, mla kobe ruksa.
Swala la uchinja lisiwe swala la serikali, hii iwe fursa kwa wafanyabiashara kwa kutambua wateja wao. Hili swala sidhani kama ni kubwa isipokuwa serikali ndiyo chanzo kikubwa. Kila raia anahaki ya kuchinja mnyama salama aliyekaguliwa. katiba haisemi nani achinje wapi na saa ngapi.

Tumeheshimiana sana, hata leo hapa kijijini kwetu bado naoana heshima ya enzi na enzi bado ipo. Ila favour ikibadilishwa sheria ndio balaa linaanza. hakuna raia namba moja wala mbili. Na kila dini ni bora kwa muumini husika.

Polisi acheni majibu mepesi kwa kuchezea imani za watu.

Chief Mkwawa
Tanganyika na Zanzibar ilikuwa na amani bila dini. Dini ni ujio wa wakoloni na waarabu. Dini za mababu zetu zilitufundisha upendo na kuheshimiana. Dini mpya zinatufundisha kuchinjana na kutukanana. Tusome upya hivi vitabu vya wageni. Vikitushinda turudi kwenye mapango yetu.
 
Osama alitafutwa miaka 10 ,taifa kubwa kama marekani,mfumo kristo hatari sana,polisi inaonekana imekufuru kwa kumjibu mungu wao pengo.
 
Ujumbe wa kuifuata njia sahihi ulishatufikia, Hatuwezi kurudi nyuma na kuanza kuabudu na kuomba mapango au binadamu wenzetu kwani havitusaidii kitu vyote hivyo viko chini ya mamlaka ya M'Mungu, M'Mungu ambaye hakuzaa wala hakuzaliwa.
 
Sikupotezei chochote kama ninaamini ninachokiabudu na siamini unachokiabudu.Cha msingi heshima juu ya imani ya mtu ni kitu cha msingi.Hakuna binadamu aliyekufa akarudi akatwambia ameona nini.Kila mtu aamini anachoamini hata kama naamini Ng'ombe,paka,mawe miti au chochote hakikutii wewe unajisi na motoni nitaenda mwenyewe.Cha msingi kaa na dini yako na mwingine akae na dini yake.Kama unauwezo wa kumbadilisha fanya jitihada za kuweka kwa nini dini yako ni bora na siyo kutukana imani au dini nyingine.

Wakristu wakianza kutukana usilamu sidhani kama Tanzania patakalika la msingi kila mtu aheshimu imani yake.Matusi na kashfa dhidi ya dini nyingine yanaudhi sana.
 
Osama alitafutwa miaka 10 ,taifa kubwa kama marekani,mfumo kristo hatari sana,polisi inaonekana imekufuru kwa kumjibu mungu wao pengo.

Kwa uelewa wangu Marakani inaendeshwa kwa siasa ya kidini na dini ya kikristu.Sioni kama kuna shida Iran,Iraq,Egypty,Afghanistan serikali zao hawa zinaendeshwa kwa kutumia sharia za kiislamu na ugomvi na vita vya wenyewe kwa wenyewe haviishi.KInachotakiwa ni kuheshimiana na kusaidiana kulijenga Taifa letu.Pale inapobidi kupeana ushauri tunapeana kama watanzania na siyo kama watu wa dini fulani.

Sidhani kama ni sahihi kusema Askofu Pengo ni Mungu wa Polisi,Askofu ni binaadamu kama wewe na mimi na anahaki ya kutoa maoni yake au malalamiko yake pale anapoona hakutendewa haki au jamii anayoingoza haikutendewa haki.
 
Polisi nao ni majangili tuu sema yamevaa sura ya serikali

hapa hakuna mlinzi Tanzania kwa hali ilivyo sasa. Tunawatu wanaoframe mipango ya kubambikia watu kesi
 
Pengo anauwezo wa kuwasiliana na polisi kujua maendeleo ya upelelezi...kwa makusudi anajaribu kuifanya nchi isitawalike! huu ni upuuzi na hauvumiliki kwa njia yoyote ile! kwanini hakutoa matamko alipouawa wananchi wa mwembe chai? mauaji ya zanzibar kule pemba yalikuwa halali? Sheikh Ponda amechoma kanisa? kesi ya ponda inauhusiano gani na vurugu za kidini? kwanini hakutoa matamko? watoto wakiislamu walipofelishwa mbona hakukemea? pamoja na kwamba kilichofanyika ni uhalifu na haivumiliki kwa jamii ya wastaarabu, bado viongozi wa dini wanapaswa kuwa na ustaarabu plus kuonyesha uvumilivu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu kwa mustakbali wa nchi yetu! ....Kwanini Pengo hakemei Mikataba mibovu ya uchimbaji madini na mauji ya wananchi wa nyamongo? Tafakari...
 
Ni kweli anauwezo huo ila ukiona hivyo ujue hakuna mawasiliano mazuri. yani anaonakama ni dana dana tuu zinaendelea
 
Pengo anauwezo wa kuwasiliana na polisi kujua maendeleo ya upelelezi...kwa makusudi anajaribu kuifanya nchi isitawalike! huu ni upuuzi na hauvumiliki kwa njia yoyote ile! kwanini hakutoa matamko alipouawa wananchi wa mwembe chai? mauaji ya zanzibar kule pemba yalikuwa halali? Sheikh Ponda amechoma kanisa? kesi ya ponda inauhusiano gani na vurugu za kidini? kwanini hakutoa matamko? watoto wakiislamu walipofelishwa mbona hakukemea? pamoja na kwamba kilichofanyika ni uhalifu na haivumiliki kwa jamii ya wastaarabu, bado viongozi wa dini wanapaswa kuwa na ustaarabu plus kuonyesha uvumilivu ikiwa ni pamoja na kufuata taratibu kwa mustakbali wa nchi yetu! ....Kwanini Pengo hakemei Mikataba mibovu ya uchimbaji madini na mauji ya wananchi wa nyamongo? Tafakari...

Unapomlaumu Askofu Pengo kwa nini hakukemea fujo na mauaji yaliyotokea Mwembechai ,unamksea haki,Je viongozi wa dini ya kiislamu/BAKWATA walipiga kelelekuhusiana na hilo.Kama hapana basi walaumu hao maana hawakutekeleza wajibu wao kwa jumuia wanayoiongoza.Anachofanya Askofu Pengo anapiga kelele na kusemea kule anakoona anaowaongoza wanahitaji kusemewa na ndiyo anawasemea.Na alichosemea siyo tu kwa ajili ya Mkatoliki bali kwa ajili ya Mtanzania yoyote apewe haki inayostahili.Na ndiyo maana amesema kikundi kidogo kinachafua dini ya kiislamu hakusema waislamu wote na ndiyo maana ameitaka serikali kukiangalia na kukionya kikundi hiki kwa faida ya muislamu na Mkristu (Mtanzania)
 
Mimi napita tu, lakini kwa mbaali nasema hivi kila zizi lina mwenyewe na mwenye zizi awajua kondoo, Mbuzi au Ng'ombe wake. Mchungaji bora ni yule asiye kaa kitako wakati walio wake katika zizi lake wanauwa kinyama. Napita tu jamani....
 
mbona viongozi waislam wanapojaribu kudai maslahi ya waislam wanaowaongoza maaskofu ndio wanakuwa kimbelembele kutoa matamko kwa jambo ambalo haliwahusu.
 
ilboru1995
....Kwanini Pengo hakemei Mikataba mibovu ya uchimbaji madini na mauji ya wananchi wa nyamongo? Tafakari...

Mkuu ilboru1995 mikataba mibovu ya madini na Pengo wapi na wapi? Kuhusu mauaji holela ya raia na ukosefu wa usalama wao ndicho anacholalamikia hapa na wewe unamlaumu kwa hilo? Au ni kwa sababu raia anayelalamikiwa ni padre ambaye wewe unamuona ni kafiri? Mkuu ilboru1995 hizi dini tuliletewa na zote zinahubiri upendo katika maisha yetu. Sasa hili la "chinja kafiri" limetokea wapi tena yarabi? Afu ni dini gani inahubiri hivyo? Kama ni uislamu ni uislamu gani huo?
 
Unapomlaumu Askofu Pengo kwa nini hakukemea fujo na mauaji yaliyotokea Mwembechai ,unamksea haki,Je viongozi wa dini ya kiislamu/BAKWATA walipiga kelelekuhusiana na hilo.Kama hapana basi walaumu hao maana hawakutekeleza wajibu wao kwa jumuia wanayoiongoza.Anachofanya Askofu Pengo anapiga kelele na kusemea kule anakoona anaowaongoza wanahitaji kusemewa na ndiyo anawasemea.Na alichosemea siyo tu kwa ajili ya Mkatoliki bali kwa ajili ya Mtanzania yoyote apewe haki inayostahili.Na ndiyo maana amesema kikundi kidogo kinachafua dini ya kiislamu hakusema waislamu wote na ndiyo maana ameitaka serikali kukiangalia na kukionya kikundi hiki kwa faida ya muislamu na Mkristu (Mtanzania)

Huo ndio utaratibu mbovu tunaopinga,suala la maauaji linapaswa kukemewa na watu wote bila kujali aliyeuawa ni wa dini gani awe mwiislam au mkristo.
 
Mkuu ilboru1995 mikataba mibovu ya madini na Pengo wapi na wapi? Kuhusu mauaji holela ya raia na ukosefu wa usalama wao ndicho anacholalamikia hapa na wewe unamlaumu kwa hilo? Au ni kwa sababu raia anayelalamikiwa ni padre ambaye wewe unamuona ni kafiri? Mkuu ilboru1995 hizi dini tuliletewa na zote zinahubiri upendo katika maisha yetu. Sasa hili la "chinja kafiri" limetokea wapi tena yarabi? Afu ni dini gani inahubiri hivyo? Kama ni uislamu ni uislamu gani huo?
Gilly nitake radhi mkuu, wewe kuwa mtoto wa mama mkubwa ingawa mdogo kwakuwa alichelewa kumpata Ishaka/Izack haikufanyi wewe kuwa kafiri! besides Muislam safi lazima asome na aelimike kwa kusoma Quran, Injil, Taurat na Zaburi. Back kwenye mada, kunauthibitisho usiokuwa na shaka ndani yake kuwa vyombo vya dola na taasisi nyingi kutowatendea haki waislam kwa kisingizio cha ugaidi, pale kisutu waislamu huwa wanadhalilishwa, Bugando mwanza waislamu sasa wanapekuliwa mpaka kwenye bikini! kuna baadhi ya ofisi hawaruhusu watu kuvaa mavazi ya heshima kama hijab!
Kanisa linasehemu yake katika mikataba mibovu madini iliyoingiwa, hili haliitaji ufafanuzi maana sote tunafahamu jinsi ambavyo linawaandaa watu wake na kuwaweka katika maeneo nyeti kama hayo... mrejesho mdogo unaotokana na mapato hayo hurejea thru NGO's. Ona walivyoshupalia chenji ya radar ipewe NGO, Ona Benjamin Mkapa alivyoanzisha NGO yake ili mgawo wake uendelee. Zile migodi zinazomilikiwa na Kanisa linawanufaishaje waumini wengine?... usiniele BAKWATA kwakuwa hata wewe unajua kuwa ni extension ya kanisa na CCM... Bahati mbaya sana kwa Watanzania ni kuwa hawajui kuwa hizi dini ziko kwa ajili ya kutupumbaza wakati wao wanaendelea kunyonya rasilimali zetu...
 
Kila kada inahaki ya kutoa tamko pale inapoona haki haitendeki. Kazi ya serikali ni kuilinda na kuhakikisha sheria zinafuatwa na wananchi wote bila upendeleo. Muuaji ni muuaji hata kama ni usalama wa Taifa, Polisi, nk . Inaonekana wauaji wapo ndani ya mfumo ndio maana kuna vigugumizi. Najua wengi kucha zetu zitaondoka bila ganzi.
 
Matokeo ya Uchaguzi mkuu 2010 bado yamemvuruga Mwadhama mwacheni Atapike Nyongo homa ipungue, Watanzania hawadanganyiki tena, Wakaristo wengi walipuuza maelekezo ya Waraka wakamimina kura zao kwa Jakaya kwa kuwa waliona upuuzi mtupu eti wamtoe Jakaya wamwingize Katibu wa Baraza la Maaskof, hata Mkapa aliwananga hadharani kuwa ni mashetani wavaa majoho wakati wa Kufunga kampen za Rais kikwete Oct 30, 2010 viwanja vya jangwani!
 
sikupotezei chochote kama ninaamini ninachokiabudu na siamini unachokiabudu.cha msingi heshima juu ya imani ya mtu ni kitu cha msingi.hakuna binadamu aliyekufa akarudi akatwambia ameona nini.kila mtu aamini anachoamini hata kama naamini ng'ombe,paka,mawe miti au chochote hakikutii wewe unajisi na motoni nitaenda mwenyewe.cha msingi kaa na dini yako na mwingine akae na dini yake.kama unauwezo wa kumbadilisha fanya jitihada za kuweka kwa nini dini yako ni bora na siyo kutukana imani au dini nyingine.

Wakristu wakianza kutukana usilamu sidhani kama tanzania patakalika la msingi kila mtu aheshimu imani yake.matusi na kashfa dhidi ya dini nyingine yanaudhi sana.
kutukana dini ya mtu ni makosa bali kumwelekeza kwa unyenyekevu aliyepotea ni maagizo ya muumba
 
Back
Top Bottom