Wauguzi katika hospitali za zamani walitambua umuhimu wa mwanga wa jua katika kuimarisha afya za wagonjwa

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787

Mwanga wa jua una faida lukuki katika mwili wa mwanadamu hasa wagonjwa. Hospitali za zamani zilikuwa na utaratibu wa kuwatoa na kuwaweka wagonjwa maeneo ya wazi ili wapate mwanga wa jua.

Siku hizi utaratibu huo haupo tena, wagonjwa wanashinda ndani kutwa nzima, hawapati mwanga wa jua kabisa.

Sio wagonjwa tu, hata watu walio wazima wa afya nao hawapati jua la kutosha, wanashinda ndani ya majengo kutwa nzima, wanaingia asubuhi na wakitoka ni usiku.

Cancer na magonjwa mengine ya ngozi yanazidi kuibuka, sababu kuu ni ukosefu wa mwanga wa jua. Tujitahidi kupata jua kadri tuwezavyo kwani ni muhimu kwa afya zetu.

☀️Jua ni tiba, jua linaponya.
 
ingekuwa ni la muhimu kihivyo wagonjwa wangekuwa wanalazwa juani mpaka hivi leo

wataalamu hawawezi kupuuzia mambo ya muhimu
Mbona sikuhizi suala la mgonjwa kufariki si la ajabu sana hasa kwenye hospitali za serikali? Hata wanawake wanavyojifungua si Kwa kuheshimiwa sana kejeri na matusi vinakuwepo hasa kabla ya magufuli na hivi Sasa hali inaanza kuwa hivyo taratibu. Foleni ni kubwa mahospitali na vyumba vya madaktari vinakuwa wazi
Madawa yanauzwa kwenye maduka binafsiya
je hizo ni taratibu za afya?
 
Siku hizi hakuna wataalamu bali wafanya biashara kwenye sekta ya afya
Wataalamu wapo, ni kwamba tu kupata tiba inabidi mtu ashiriki kwenye mfumo wa ubepari(manunuzi) uliopo.

Lakini tiba ipo hospitalini ingekuwa watu wanakufa tu kule nani angekuwa anaenda? Pata tatizo dogo tu kama ghonorrhea halafu usizingatie hospitali uone.
 
Sawa, turudi kwenye mada.

Jua ni muhimu na kulikosa ni kujisogeza karibu na magonjwa hasa cancer ya ngozi.
 
Mifumo ya usambazaji tiba ndo inashida lakini tiba ya uhakika ipo
 
Siku hizi hawataki tupone maana tukipona kabisa biashara yao itakosa soko.
hakuna mtu anayetaka kupona mitindo ya maisha tu unajionea mwenyewe

na bado kuna yale magonjwa ambayo hayakwepeki, unaweza pata muda wowote au kwasababu ya uzee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…