Mgomo wa wauguzi na wakunga nchini Kenya umeendelea kuathiri huduma katika hospitali za umma huku kukiwa na ripoti za vifo vya kina mama na watoto.
Kulingana na taarifa kutoka kwa mashirika ya wataalamu wa afya, vifo 79 vilirekodiwa kati ya Septemba 1 na 3, 2026. Takwimu hizo zinajumuisha vifo 8 vya kina mama, 16 vya watoto wachanga na 55 vya watoto katika kipindi cha uzazi (perinatal deaths).
Takwimu za EWENE pia zinaonyesha kuwa vifo 130 vya perinatal viliripotiwa kati ya Agosti 24 na 30, huku vifo 44 vya watoto wachanga vikirekodiwa katika kipindi hicho. Video inaonyesha maandamano ya wauguzi huku wakishinikiza serikali kushughulikia madai yao.
Mgomo huo ulianza Julai 29, 2026, huku wauguzi wakitaka utekelezaji wa makubaliano ya kazi (CBA), utekelezaji wa makubaliano ya kurejea kazini ya 2017, pamoja na ajira ya kudumu kwa baadhi ya wafanyakazi wa UHC.
Kisumu, Nakuru, Kakamega na Kajiado ni miongoni mwa kaunti zilizoripoti idadi kubwa ya vifo. Wataalamu wa afya wameonya kuwa kuendelea kwa mgomo kunaathiri pia wagonjwa wanaohitaji kulazwa, huduma za uzazi na matibabu maalumu kama dialysis.
Muungano wa wauguzi, hata hivyo, umesisitiza kuwa mgomo utaendelea hadi madai yao yatakaposhughulikiwa.
Source : Thestandard