ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Wauguzi wa afya wametakiwa kuimarisha mawasiliano bora na wagonjwa pamoja na kuzingatia miongozo ya kitaaluma badala ya kufanya kazi kwa mazoea, ili kuboresha utoaji wa huduma za afya na kuhakikisha mgonjwa anahudumiwa kama mteja mwenye thamani.
Hayo yamebainishwa kupitia mafunzo maalumu ya kuimarisha na kuboresha huduma kwa wagonjwa yanayotolewa kwa wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mt. Joseph Peramiho iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea, mkoani Ruvuma. Wauguzi walioshiriki mafunzo hayo wamesema yamewasaidia kutambua wajibu wao katika kuhudumia wagonjwa kwa weledi na kwa kuzingatia miongozo ya afya.
Wamesema kuwa mafunzo hayo yamewaongeza uelewa juu ya umuhimu wa kumheshimu mgonjwa kama mteja, kumjali, na kumpa huduma kwa wakati bila kutumia mazoea au utaratibu usiozingatia taaluma.
Kwa upande wao, wakufunzi wa mafunzo hayo wamewahimiza wauguzi kuendelea kuthamini mchango wa wagonjwa katika mchakato wa huduma za afya. Wamesisitiza kuwa utamaduni wa kumhudumia mgonjwa kama mteja unasaidia kuondoa malalamiko ya wananchi kuhusu dhana kuwa wauguzi hawatoi huduma bora.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mt. Joseph Peramiho, Dkt. Deodatus Haule, amesema uongozi wa hospitali umeandaa mafunzo hayo ya siku tatu kwa lengo la kuboresha zaidi utoaji wa huduma kwa wagonjwa. Amesema kwa sasa huduma za afya zimeenea na uwezo wa watoa huduma umeongezeka, hivyo ni muhimu kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa kuzingatia weledi, maadili na mawasiliano mazuri.
Dkt. Haule ameongeza kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa hospitali katika kuboresha mazingira ya utoaji huduma na kuongeza uaminifu wa jamii kwa watoa huduma.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuleta mabadiliko chanya katika namna wauguzi wanavyowahudumia wagonjwa na kukuza uhusiano mzuri kati ya wahudumu na jamii.