DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kesi ya Kikatiba nambari 16408 ya Mwaka 2025 iliyofunguliwa na waumini 52 wa kanisa la Ufufuo na Uzima (Glory Of Christ Tanzania Church) inatarajiwa kuanza kusikilizwa leo Julai 11, 2025 katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu inayoketi Dar Es Salaam.
Waumini hao 52 wanadai kufanyiwa vitendo visivyo sawa kisheria ikiwemo kupigwa juni 29, 2025 wakati wakifanya ibada.
Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, ambapo waumini hao waliwasilisha shauri hilo Mahakamani chini ya hati ya dharura iliyosainiwa na Wakili Peter Kibatala wakiieleza Mahakama kuwa udharura wa kesi unatokana na shauri hili linagusa haki nyeti sana ya Uhuru wa Dini, na wa kuabudu.
Na sababu nyingine iliyoelezwa ya udharua ni haki za kidini za walalamikaji, ambazo wanadai zimekiukwa na vitendo vya Mjibu Maombi wa Pili, Inspekta Jenerali wa Polisi, zitaendelea kuwa hatarini hadi pale shauri hili litakapopatiwa uamuzi.
Waumini hao 52 wanadai kukamatwa na Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam mnamo Tarehe 29 Juni 2025 katika eneo la Ubungo wakati wakitekeleza haki yao ya Kikatiba ya kuabudu na kuumini, Haki ambazo zimejengwa katika Ibara ya 19 [1] ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
Wanaitaka Mahakama Kuu itamke kwamba Jeshi la Polisi limevunja Haki zao za Kikatiba kwa kuwakamata wakiwa Ibadani, na kuwaweka kizuizini katika Kituo cha Polisi Oysterbay bila kuwa na msingi kisheria.
Kesi hiyo inasikilizwa na Jopo la Majaji Watatu, ambao ni Mkeha, Maruma na Kisanya.