Waumini wa Gwajima watakiwa kusalia nyumbani

Waumini wa Gwajima watakiwa kusalia nyumbani

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,922
Reaction score
3,252
Katibu mkuu wa Kanisa la Glory of Christ (Nyumba ya Ufufuo na Uzima), Dk Erick Shoo ametangaza kutokuwa na ibada katika matawi yote ya kanisa hilo leo Juni 8, 2025 ikiwa ni utekelezaji wa kufungwa kwa kanisa hilo.

Hivyo Dk Shoo amewataka waumini hao kuabudia kila mtu nyumbani kwake hadi watakapotangaziwa tena.

Juni 2, 2025 Msajili wa Jumuiya za kiraia, Emmanuel Kihampa alitoa tangazo la kulifungia kanisa hilo akitoa sababu za Askofu wa Kanisa hilo, Josephat Gwajima kuchanganya dini na siasa.

Hatua hiyo ilifuatia kauli za Gwajima kufanya mkutano na vyombo vya habari akieleza kuwepo kwa matukio ya utekaji na katika ibada ya Juni 1, 2025 makao makuu ya kanisa hilo alisisitiza kauli zake hizo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Juni 7, 2025 jijini hapa, Katibu mkuu wa kanisa hilo, Dk Shoo amesema hakutakuwa na ibada katika makanisa yote na wala hakutakuwa na huduma za kufungisha ndoa, ubatizo wala meza ya Bwana.

Angalia video.

Pia soma ~ Waumini wa Kanisa la Gwajima wafanya maombi na Ibada nje ya Kanisa hilo Ubungo
 
Back
Top Bottom