Waumini Wa Mwamposa Moshi Wasema''Alituponya hata kesho akija tunaenda

Waumini Wa Mwamposa Moshi Wasema''Alituponya hata kesho akija tunaenda

Dini ndio “Bangi” kubwa ya walala hoi very simple logic anayeponya si mwamposa bali ni Mungu Mwenyewe na cha pili hasa ni mtu mwenyewe kupata kibali cha uponyaji au kufunguliwa .
Maarifa ni jambo muhimu sana na kumcha Bwana ndio chanzo cha maarifa wengi huchukia maarifa kwa kuwa wamekataa ufahamu.

Hizi mambo za mitume sijui manabii sijui wachungaji si lazima katika kutimiza uponyaji au kufunguliwa kwa mtu kwa maana alipokufa Yesu msalabani tendo moja wapo kuu lililofanyika ni kupasuka kwa pazia lilokuwa linatengenisha patakatifu(hapa watu wote waliweza kufika na kuwasilisha maombi na zaka zao) na patakatifu pa patakatifu (hapa aliingia kuhani mkuu pekee ili kuwasilisha zaka,maombi na sadaka za watu) kwa maana hii kila aliyeamini na kukiri amepata kibali cha kuliita jina la Mungu katika maisha yake na kupokea hitaji la moyo wake sawa sawa na mapenzi ya Mungu yaliobeba kusudi katika maisha ya mtu husika.

Uponyaji na miujiza ni sehemu ambayo imechukua watu wengi waliokosa ufahamu tokea enzi kuna nyakati kwenye biblia alitukia jamaa aliyeitwa Bal-Yesu huyu alitumia nguvu za giza kufanya uponyaji na miujiza lakini mitume wakafahamu kwakuwa walikuwa na nuru iliyoletwa kwa wao kujawa na maarifa.
Hutaweza kupambanua haya mambo kama hauna maarifa na neno la Mungu kukaa ndani yako utalishwa mpaka sabuni ukiambiwa inaondoa mikosi.

Mpende bwana Mungu wako kwa akili zako zote ,Akili ni kitu au nyezo muhimu katika Kumpenda Mungu.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
u kwakuwa walikuwa na nuru iliyoletwa kwa wao kujawa na maarifa.
Hutaweza kupambanua haya mambo kama hauna maarifa na neno la Mungu kukaa ndani yako utalishwa mpaka sabuni ukiambiwa inaondoa mikosi.
YESU aliponya kwa kutumia hadi mate na matope na watu walimfuata hawakuacha kumfuata sembuse kutumia sabuni
 
Watu wameshasahau tena kisali kwa Mungu wao, wamebaki kuzunguka kutafuta miujiza, inasikitisha sana. Ila sio mbaya maana wanasema kuwa 'what matters is what you believe'. I
sidhani kama una jua ila
Wengi wanaoenda huko wana matatizo makubwa na hawana choice na wengine wanapona amini usiamini.

"Ceteris Paribus"

Kuna baadhi ya watu wameshazunguka Hospitali zote na hawajapata tiba.
Hawana kimbilio zaidi ya kuzunguka kwenye wachungaji na manabii .

Na kuna shuguda watu wanapona.
Mimi nimeona kwa macho yangu.

Maombi huponya. Japo hutaweza kuona kila mtu akipona haiwezekani.

Kwa hio msiwabeze watu.

Siku ukipigwa na gonjwa ( japo sikuombei) ndio utajua ninachojaribu kukueleza.
 
Tuache watu na imani zao hivi mnadhani wangekuwa hawaponywi wangejazana pale kawe kwenye huduma yake?Watu wanatembea kwa umbali mrefu kutafuta usafiri wa kwenda kawe kukanyaga mafuta tu haijalishi ni ya kichawi au kiMungu lkn watu kwa imani zao wanapona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuache watu na imani zao hivi mnadhani wangekuwa hawaponywi wangejazana pale kawe kwenye huduma yake?Watu wanatembea kwa umbali mrefu kutafuta usafiri wa kwenda kawe kukanyaga mafuta tu haijalishi ni ya kichawi au kiMungu lkn watu kwa imani zao wanapona.

Sent using Jamii Forums mobile app
hawaelewi hao mwenye shida hachagui mganga
 
Watu wameshasahau tena kisali kwa Mungu wao, wamebaki kuzunguka kutafuta miujiza, inasikitisha sana.
Wana mahitaji majibu hamna .Hata waislamu wanaitafuta sana ona hapa.

Waziri wa Mambo ya ndani Simbachawene kazi unayo

 
Back
Top Bottom