Jamani watu wanamatatizo, Tena wengine ni makubwa sana. Kwa hiyo nahisi watu wanatafuta faraja popote ilipo haijarishi ni wapi, iwe kwa mwamposa, ngwajima ama yoyote yule ama popote pale hata iwe kwa waganga, kwa hiyo mtu akipata pakujifariji na kujipa hope mambo yatakaa sawa ama kama ni ugojwa utapona ama kama ni kipato Basi si mbali mambo yatajipa, kifupi liwe tatizo lolote ambapo anaamini kupitia kwa huyo mtu ama hapo mahali Basi hayo matatizo yanayomkabili yataisha ama kupungua, kwa Kweli mtu akipata hiyo faraja, kwa Kweli huna cha kumueleza akakuelewa. Eti uje umwambie "hayupo mahali sahihi" sasa atakuuliza ni wapi mahali sahihi kwa kimbilio la matatizo yake?!....uwe na jibu sahihi la kumueleza
Hitimisho ni kwamba watu wamefanya MATATIZO YA WATU KAMA MTAJI na wanajua hawa watu hawana ujanja.