Dini ndio “Bangi” kubwa ya walala hoi very simple logic anayeponya si mwamposa bali ni Mungu Mwenyewe na cha pili hasa ni mtu mwenyewe kupata kibali cha uponyaji au kufunguliwa .
Maarifa ni jambo muhimu sana na kumcha Bwana ndio chanzo cha maarifa wengi huchukia maarifa kwa kuwa wamekataa ufahamu.
Hizi mambo za mitume sijui manabii sijui wachungaji si lazima katika kutimiza uponyaji au kufunguliwa kwa mtu kwa maana alipokufa Yesu msalabani tendo moja wapo kuu lililofanyika ni kupasuka kwa pazia lilokuwa linatengenisha patakatifu(hapa watu wote waliweza kufika na kuwasilisha maombi na zaka zao) na patakatifu pa patakatifu (hapa aliingia kuhani mkuu pekee ili kuwasilisha zaka,maombi na sadaka za watu) kwa maana hii kila aliyeamini na kukiri amepata kibali cha kuliita jina la Mungu katika maisha yake na kupokea hitaji la moyo wake sawa sawa na mapenzi ya Mungu yaliobeba kusudi katika maisha ya mtu husika.
Uponyaji na miujiza ni sehemu ambayo imechukua watu wengi waliokosa ufahamu tokea enzi kuna nyakati kwenye biblia alitukia jamaa aliyeitwa Bal-Yesu huyu alitumia nguvu za giza kufanya uponyaji na miujiza lakini mitume wakafahamu kwakuwa walikuwa na nuru iliyoletwa kwa wao kujawa na maarifa.
Hutaweza kupambanua haya mambo kama hauna maarifa na neno la Mungu kukaa ndani yako utalishwa mpaka sabuni ukiambiwa inaondoa mikosi.
Mpende bwana Mungu wako kwa akili zako zote ,Akili ni kitu au nyezo muhimu katika Kumpenda Mungu.
Sent from my iPhone using JamiiForums