Wauza magenge hili linawahusu

Joined
Jul 19, 2022
Posts
64
Reaction score
89
Wauza magenge hasa wauza dagaa kuna kero huwa mnanipa sijui ndiyo mnawahi muda au ubize. Kitendo cha kupima dagaa au samaki waliokaangwa kwa mkono ambao haujavaa chochote au haujatumia kitu chochote kupima hizo dagaa kweli imekuwa ni kero na imefanya kugombana na wauzaji wengi.

Ushauri wangu kwa ambao mnafanya hivyo muache, maana hatujui kabla ya kupima hizo dagaa mkono wako ulishika nini. Pia nimeonesha wanaovaa vitu vya kushikia.
 
Umeongea sahihi hio ni asili ya uchafu ....ukute muuzaji katoka kujikuna mahali....sema ndio hivyo Mungu hutulinda tu ila wauza dagaa wengi wachafu sana
 
Hapo ulichoona ni final tu huko nyuma tangu kuvuliwa, kusafishwa, maji yaliyotumika, vyombo vilivyotumika, sehemu zilipohifadhiwa, mafuta yaliyotumika ni majanga tupu
 
unajali kuhusu mkono ilihali hao dagaa ako wazi na wanang'ong'wa na ma-inzi ?

navyojua ukiwanunua , ni kuwapasha kabla kula

kufata protokalo za ki-hygiene eneo la uswazi sahau
 
unajali kuhusu mkono ilihali hao dagaa ako wazi na wanang'ong'wa na ma-inzi ?

navyojua ukiwanunua , ni kuwapasha kabla kula

kufata protokalo za ki-hygiene eneo la uswazi sahau
Ni kweli mkuu,hizo protocol ni za kwenye Mall/Supermarket.
Uswazi kuna mambo mengi sana hilo la kushika na mkono ni jambo dogo mno ukilinganisha na mambo mengine kwa mfano mazingira anakokaanga hao samaki hujui pakoje,vyombo anavyotumia hujui vikoje.
 
Aedes
 
Sina hamu na hao dagaa wa maji chumvi..kuna siku nilikua geto nikawa na hamu na dagaa sana..nikaenda nikanunu kama fungu mbili hivi nile na dona yangu na mtindi.

Nimewaanda vzr rosti tia ndimu za kutosha..nikala na ugali huku nashushia na mtindi..ile na maliza tu daah nilianza kujihisi kichefuchefu balaa..acha nitapike daah sitasahau siku hiyo..hao dagaa nmewachukia kweli toka siku hiyo sijui walikua na shida gani.

Bora ni nunu dagaa wa mwanza.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Tafakari shida zako. usisingizie dagaa.
 
Kwa mchanganyiko huu utaachaje kutapika[emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…