DOKEZO Wauza michele SIDO - Mbeya hatujapata Mkopo wa Mama Samia mwaka na zaidi sasa kisa uongozi wa Soko

DOKEZO Wauza michele SIDO - Mbeya hatujapata Mkopo wa Mama Samia mwaka na zaidi sasa kisa uongozi wa Soko

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mwaka jana miezi kama hii walitutembelea maofisa wa bank ya CRDB tawi la Livingston na kutushauri kutuongezea mtaji kwa kutupa mikopo, sisi wafanyabiashara wa hali ya chini tulichangamkia fursa kwa kwenda bank kufungua account na kupata fomu za mkopo huo ulioitwa mkopo wa Mama Samia

Matokeo yake ni mwaka na zaidi sasa hizo fomu hazijafika bank na zipo kwa viongozi wa soko na tunajibiwa kuwa sisi ni wachanga hatuwezi kupewa mkopo, na majibu haya anayatoa kiongozi wa soko upande wa MBEYA RICE anayeitwa Kabosi. Maajabu yake hao viongozi wa soko kila wakati wanakopa kwenye mabank balimbali.

Huyu kiongozi wa soko ambaye fomu zipo ofisini kwake ametukwamisha mambo mengi maana wafanyabiashara hawa wadogo walikuwa wanachukua mikopo kwenye taasisi nyingine na wakaachana nazo kwa kutegemea mikopo ya crdb, na kuendelea kusubiria mkopo wa CRDB uliokwama mwaka na kitu sasa

Huyu kiongozi wa soko Kaboss amegoma kabisa kutusainia mikopo yetu na kakaa na fomu ofisini kwake.

Tunakuomba mbunge Tulia na Rais Samia utusaidie kwa hili kwani kwenye masoko mengine wameishapata muda mrefu

Ni sisi wafanyabiashara wa mchele mashine za mpunga Sido Mbeya
 
Back
Top Bottom