Wauza nyama Nyanda za Juu Kusini wapigwa marufuku kutumia magogo buchani

Wauza nyama Nyanda za Juu Kusini wapigwa marufuku kutumia magogo buchani

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wafanyabiashara na wamikili wa maduka ya nyama mikoa ya nyanda za juu kusini, wametakiwa kuzingatia maagizo ya Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) kutumia vifaa maalum vya kukata nyama na kuachana na matumizi magogo ya miti ili kulinda afya za walaji.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 13,2023, Ofisa mifugo bodi ya nyama Kanda Dk Mpoki Alilanuswe amesema tayari miongozo na maelekezo vilitolewa na kilichofuata ni utekelezaji na kwamba matumizi ya magogo ya miti yanaweza kuleta madhara kwa walaji wa mwisho.

“Sekta ya nyama ni sekta nyeti ambayo inahitaji umakini mkubwa kuanzia hatua ya uandaaji kutoka kwenye machinjio mpaka sokoni sasa tunapotoa maelekezo lengo ni kuwepo kwa ubora wa kitowei hicho kwa walaji,”amesema.

Dk Alinanuswe amesema katika kukabiliana na hali hiyo bado wanaendela kuhamasishaji matumizi ya vifaa vya kisasa kuandaa nyama, ikiwepo magogo ya plastiki wakati wa kukata kitoweo hicho kabla ya bodi kuanza kuchukua hatua za kufanya ukaguzi.

Wakati huo huo ameomba Serikali na wadau kuwekeza nguvu kuboresha machinjio na uanzishwaji wa viwanda vidogo vya kusindika nyama ili kusafirisha kupata masoko ya nje ya nchi kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe (SIA) .

“Nyanda za juu kusini kuna kiwanda kimoja cha usindikaji wa nyama ambacho asilimia kubwa wanategemea masoko ya ndani kutokana na kutokidhi vigezo vya kusafirisha nje ya nchi hivyo kuna uhitaji wa nguvu ya serikali na wadau katika uwekezaji kwani uhakika wa mifugo ni mkubwa ”amesema.

Mfanyabishara wa duka la nyama, Nassoro Nassoro amesema changamoto kubwa ya kufikia malengo ya utekeleza ni kutokana na baadhi yao kuwa na mitaji midogo ambapo matumizi ya vifaa vya kisasa kucharangia nyama vinahitaji rasirimali fedha.

“Tunaomba Serikali itusaidie kupata mikopo ya vifaa hivyo ili tuweze kwenda na teknolijia za kisasa za uandaaji wa nyama kwa lengo la kulinda afya za walaji wa chini ,sambamba na kutenga maeneo maalum kwa ajili ya maduka husika. ”amesema.

Mkazi wa Jijini Mbeya, Salome Joel ameiomba TMB kuweka msisitizo wa kupiga marufuku kutumia magogo ya miti kukata nyama kutokana na madhara kiafya kwani yamekuwa sio salama kutokana na kutofanyiwa usafi .
 
Mbona afadhali gogo la mti kuliko gogo la plastic kiafya? Sioni kama gogo la mti linaweza kuleta adhari kwa afya ya binadamu ila plastics zina madhara!!

Labda watuambie ni kwanini gogo la plastic na siyo la mti?
 
Hivi hayo magogo ya plastic, yanaweza kuhimili kubondwa kwa mfupa? Bora wangesema hata magogo ya miti ila yaliyotengenezwa kwa mafundi na kuwa bora, au pia labda ya chuma.

Kwa plastic hapo ni uongooo.
 
Back
Top Bottom