Nataka S8+ SM G955U offer 450k
kwa nn usichukue SM-G955F/FD(D for dual sim) Ambayo ni global/international Model?
Hio SM-G955U ni USA-Unlocked,
kuna uwezekano ikakusumbua Network strength sbb umebadilisha zone.
Hii kitu watu wanachukulia poa ila ni vizuri sana ukinunua simu kujua model na zone yake hasa samung ambao hutengeneza simu kuendana na zones,
Japo models zinazoishia na ...U au ...0 angalau ila best ni F/FD/DS....
Hizo ndio international na hata uende nchi gani utaitumia km ilivyo na haisumbui network n.k
Ukiona Samsung mwishoni mwa model(kwa wale amabao hawajui model hua inaanza na SM-G/N/J/A halaf number km tatu hv then hizo zones/carrier sasa kamaF/DF/DS/V/A/Z n.k,
e.g SM-G955F/DS) inaishia na
A, Z, N, P, V, W, R4
jua umeuziwa carrier unlocked,
na kwa vyovyote vile itakua ni used...
Yaani ni kama vile huku kwetu, Tigo anaingia ubia na Tecno amsaidie kutangaza na kuuza simu zake kwa bei ya chini, lkn tigo nae ana mpa mashart lazima Hii simu Tui LOCK kwa laini yetu,
kwaio unaenda Tigo Shop kununua simu ya tecno(mara nyingi tunasikia zinatangazwa na tigo),
na Moja ya mashart ni kwamba lazima laini moja iwe ya Tigo(hii ndio carries LOCKED sasa)
Ukitaka kutumia laini zote basi utalazimika kwenda kwa wa taaalam wai UN-LOCK(sisi tunaita ku flash japo sio lugha sahihi sana maana lugha nzuri ni ku unlock, neno ku flash hii lugha miaka ya nyuma kdg ilikua common sana kpnd kile tunanunua vile vi simu ya vodafone n.k)
Sasa hizo simu zenye hio Models hapo juu
Mfano ukaona inaishia na V, T au A
inamaanisha ni Verizon, T-Mobile au AT&T respectively,
Hio ni mitandao ya simu ya specificaly Marekani Km sisi tunavyosema vodacom, tigo Airtel iliyoingia ubia na samsung watengeneze simu maalum kwa mitandao yao,
mashart wanayowapa samsung ni kwamba simu zao ziuzwe kwa bei nafuu na pia zifungwe zitumie lain moja ya mtandao husika.
Kwahio samsung wao wanafaidika kwa simu zao kuuzwa kwa urahisi na haraka sbb ya matangazo mengi na upatikanaji rahisi(hili tunaona kila siku tigo wakitusumbua kwenye matangazo yao kununua sijui tecno gani huko kwa bei nafuu),
Na Mtandao husika nao unafaidika kwa kupata Wateja weng maana watu watafuata kilichorahisi na itabidi wafuate mashart ya kutumia laini ya wauzaji kwa angalau miaka miwili, sbb walikuuzia kwa bei chee
Kwa hio ikishaisha ile miaka miwili(mtumiaji lazima ufuate taratibu/mkataba ukikiuka uka i flash kabla ya miaka iliyowekwa ni kosa) ndio unakuta mtu anaweza kui Unkock,
Sasa mtu akiichoka anataka kuiuza ije mara nying africa atalazimika ku i unlock kama tunavyoita ku flash, halaf inaletwa huku...
Ndio unauziwa ww,
kwaio piga ua hio simu lazima iwe used haijalishi kwa mda gani ila nyingi ni miaka miwili na kuendelea.
Lakn hii haimanishi hizo
F/FD/DS basi zote Ni mpya....
Cha kuelewa tu ni kwamba hizo zinatumika kimataifa na zinatumia laini zote,
kwaio pia mtu anaweza itumia ktk nchi nyingne akaiuza ikaja huku.
Kingne ambacho nakisema humu hii ni mara ya tatu..
Simu hizi blands kubwa na high ends kuipata mpya kbsa zaidi ya miaka miwili baada ya kutoka kiwandani ni nadra sanaaaaa.....
nyingi ni refub, mtumba nacarrier unlocked
na ukiiona hutaamini..
Au unauziwa simu hasa samsung na iphone unaona kwa ubavuni(Sio kale ka nyuma kenye model na imei) umewekewa ka sticker flan hivi half unaambiwa ni Brand New.....
Hahaaa my friend..........anza kutumia akili yako vzr...
Ulishajiuliza kwa nn max warrant hua ni miaka miwili?
Akili kwako...
Za kuambiwa changanya na zako ....
Neno langu si sheriaaa.....
upendo na amani.