Wauza tiketi wa usafiri wa Mwendokasi wanakera sana

Wauza tiketi wa usafiri wa Mwendokasi wanakera sana

Kasiano Muyenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2018
Posts
13,858
Reaction score
22,729
Siamini kabisa kuwa Udart wanaweza kuendesha biashara kwa kukosa chenji ya kurudisha kwa abiria wao.

Mara nyingi sana utakutana na kero la kukosekana chenji kwenye vile vibanda vya wauza tiketi vilivyoko kando ya barabara ya Morogoro hasa kwa maeneo ya Kimara Temboni, Mbezi kwa msuguri, Kibamba, Kiluvya nk.

Wakatisha tiketi wana sura ngumu, majibu ya nyodo, kebehi, dharau, huwa wanajibu kwa sauti kubwa HAKUNA CHENJI kisha wanatazama pembeni.

Hivi ni kweli wakatisha ticket Udart wanakosaga chenji? Kwa nini wakose chenji?
 
Kweli huu nao uzi? Wewe unatumia Jamiiforum halafu haufahamu kuwa tiketi ya mwendokasi unaweza kuipata kielektroniki kupitia Dar City Navigator app? Watanzania tuache kulalamika vitu vidogo vidogo kama chenchi badala yake twende cashless. Magufuli terminal, Benjamin Mkapa Stadium na Vivuko vya Kigamboni wanatumia kadi ni mwendo wa cashless tu.

Gavana wa BOT alishasema gharama ni kubwa kutengeneza noti na coins, watumiaji wajikite kwenye cashless halafu anatokea Great Thinker mmoja analalamika sijui dharau, kejeli na kitu gani, which can not be proved.
 
Hii nchi kila mtu anafanya anavyotaka ktk eneo lake la kazi na hamna mtu wa kumfanga chochote. Utashangaa pale kimara kuna madirisha manne ya kuuzia ticketi lkn dirisha moja tu ndo lina foreni ndefuuu!

Ukienda dirisha ambalo halina foreni eti anakujibu kirahisi tu, siuzi ticket za kwenda sehemu x, nenda kapange pale kwenye foleni ndefuuu! Hawa wasimamizi sijui wanatembea na wafanyakazi mpaka wanashindwa kuwasimamia au sijui ni kitu gani. Kesho mtu anatumbulia anaanza kulia lia.
 
sasa wakileta tiketi za kielektroniki zile za kwao za kwenye mandoo watapata wapi maokoto? muwe mnafikiaria wakati mwingine kimsingi huo ni upigaji wa kimtindo watu wanaishi mjini buana, we hujawahi kujiuliza kwanini waliwapiga chini max malipo ili watumie mikaratasi tena bila aibu katika karne hii ya kidijitali?
 
Max malipo walipigwa chini na Serikali kwa sababu waliipiga Serikali
 
Benjamin Mkapa Stadium na Vivuko vya Kigamboni wanatumia kadi ni mwendo wa cashless tu.
Bandiko halihusiani na hayo ulioandika, kuna vibanda vya kukatia tiketi kando ya barabara na ndio mada yenyewe, Udart waliweka hivyo vibanda ili wauze tiketi ila hawana chenji.

So jitahidi uelewe kuwa mambo ya kutumia kadi hata mwendo kasi wenyewe hawayawezi maana mabasi yenyewe ni mitumba, mashine za kusoma kadi hazimo ama zimekufa ndani ya mabasi yao.

Mambo ya kadi bado sana kwa mabasi ya mitumba.
 
Utashangaa pale kimara kuna madirisha manne ya kuuzia ticketi lkn dirisha moja tu ndo lina foreni ndefuuu! Ukienda dirisha ambalo halina foreni eti anakujibu kirahisi tu, siuzi ticket za kwenda sehemu x, nenda kapange pale kwenye foleni ndefuuu!
Wanakeraa
 
Kweli huu nao uzi? Wewe unatumia Jamiiforum halafu haufahamu kuwa tiketi ya mwendokasi unaweza kuipata kielektroniki kupitia Dar City Navigator app? Watanzania tuache kulalamika vitu vidogo vidogo kama chenchi badala yake twende cashless. Magufuli terminal, Benjamin Mkapa Stadium na Vivuko vya Kigamboni wanatumia kadi ni mwendo wa cashless tu.
Gavana wa BOT alishasema gharama ni kubwa kutengeneza noti na coins, watumiaji wajikite kwenye cashless halafu anatokea Great Thinker mmoja analalamika sijui dharau, kejeli na kitu gani, which can not be proved.
Kwa asiyekuwa na smartphone je ndugu great thinker?
 
Siamini kabisa kuwa Udart wanaweza kuendesha biashara kwa kukosa chenji ya kurudisha kwa abiria wao.

Mara nyingi sana utakutana na kero la kukosekana chenji kwenye vile vibanda vya wauza tiketi vilivyoko kando ya barabara ya Morogoro hasa kwa maeneo ya Kimara Temboni, Mbezi kwa msuguri, Kibamba, Kiluvya nk.

Wakatisha tiketi wana sura ngumu, majibu ya nyodo, kebehi, dharau, huwa wanajibu kwa sauti kubwa HAKUNA CHENJI kisha wanatazama pembeni.

Hivi ni kweli wakatisha ticket Udart wanakosaga chenji? Kwa nini wakose chenji?
Mfumo wa e-ticket ulikuwa unazuia wizi. Ila kwa sasa wauza ticket ni matajiri. Dkt Samia anahujumiwa!
 
Hizo tiketi hawawezi kuzitumia, kwanza haziendani na mifumo ya kupanda basi huku mnagombana na kusukumizana
Nilikua nawaza kwanini kusiwe na mfumo wa kuswap card au simu ukipanda gari kumbe magari hayana hiyo mifumo. Poleni mnaotumia huo usafiri
 
Nilikua nawaza kwanini kusiwe na mfumo wa kuswap card au simu ukipanda gari kumbe magari hayana hiyo mifumo.
Hayo magari ni ya kishsmba mno, hayana mfumo wa GPS, bell 🛎 hazifanyi kazi, yanajaza abiria kama ng'ombe wapelekwao machinjioni, hayana kiyoyozi, so mambo ya kuswap card hayawezi kuwemo ktk hayo magari
 
Mfumo wa e-ticket ulikuwa unazuia wizi. Ila kwa sasa wauza ticket ni matajiri. Dkt Samia anahujumiwa!
Mbongo hazuiliki kazaliwa kupiga kama control number tu watu wanapita nazo sembuse e tiketi.
Hakuna kitu chepesi kuiba au kuchezea kama mfumo wanacheza na weakness yake wanapitia humo humo
 
Back
Top Bottom