DOKEZO Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani

DOKEZO Wauzaji wa nyama Mbezi Beach kuna michezo wanafanya kwenye mizani

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kuna siku nimeingia bucha nakutana na mshikaji kanunua nyama kilo kumi maini kilo tano samaki kanunua yule mkubwaaa mashine ziko busy kukata nyama zake mm muuza ananiuliza bro unataka nyama kias gani nikamwambia kg moja akaniambia subiri tumalize kumkatia huyu jamaa tutakuhudumia niliondoka maana mzigo nilikuta ndo wanapigiana mahesa na ndo wameanza kukata
ndugu, tuombe tu Mungu atusaidie tupate pesa. ukiona unapambania gram 200 ya nyama buchani, ni hali ya chini ya maisha, umasikini. tupambane tutafute maisha. kuna mwaka nilikuwa naenda kununua nyama buchani nusu kilo, ila ukifika pale utakuta kuna mtu ananunua kilo 10 za nyama, na kilo kama 2 za maini. hadi mwenye busha anaona kama wewe wa nusu kilo unamsumbua vile. cha kushukuru Mungu, nilipita level hizo, na mimi napita kununua kilo 10. au samaki kilo 10, na nawaona wenzangu wananunua utumbo nusu kilo vilevile.
 
Hongera sana kwa kutoboa maishani lakini mawazo yako hayafai na hayana uhalisia katika maisha. Hata ufanye nini hakuna siku watu wote watakuwa kama nyinyi wenye uwezo wa kununua kilo 10. Actually hakuna nchi ya hivyo. Hata Marekani na Ulaya. Hii ni kwa sababu mifumo ya uchumi haijasukwa ili kuwawezesha watu wengi kuwa na uwezo wa kununua kilo 10. Kwa hiyo suluhisho lako ni butu maana hata iweje wanunuzi wa nusu kilo watakuwepo tu; na tena ndiyo wengi.

Kinachopiganiwa hapa ni kutenda haki, si katika nyama tu bali katika nyanja zinginezo maana tunayo jamii ambayo inawaza wizi tu karibu katika kila kitu. Jamii ya aina hii ni jamii iliyopotea; na kamwe haitakaa iendelee.

➡️➡️➡️ Tuweke juhudi katika kupambana na wizi huu haijalishi kama mwizi ni waziri aliyefisadika na kujichotea mabilioni au muuza nyama anayemuibia Mtanzania mwenzake gramu 200!
 
Almost sehemu nyingi sana wanaiba aisee.....kuna haja wataalam wa vipimo wafanye suprise inspection na wawapige faini za kutosha
 
Mfano mzuri ni Kigamboni kuna bucha wanauza nyama Kg 1 Tsh 8000 wengine 10,000 na kote nilishanunua sana.

Lakini siku moja ilinifikirisha sana nikajiuliza kwanini inakuwa hivi? Nilifanya uchunguzi wangu binafsi na ulilenga kwenye Ubora, wingi, stake na mifupa + huduma.

Kuanzia hapo hadi sasa na ninachoweza mshauri mtu anunue nyama ya bucha za Tsh 10,000. that is my advice.
 
Tandika nilienda kununua ubuyu wanapima kwenye mzani wa namba sasa ubuyu robo ni 1000 nikampa buku sasa nashangaa anapima 200g nikamuuliza ubuyu robo ndo gram 200? akasema aah ndo tunavyopimaga ngoja nikuongezee nikamwambia huo unaoongeza ni wangu hunipi bure fanya chap weka 250 nisepe akaweka 250g nikaamsha sasa nikajiuliza ni watu wangapi wanapimiwa kiwizi hivi hata huko buchani inawezekana watu hawajui kusoma vipimo nyama kilo anakupimia 800g
 
Mabucha mengi ni wezi wakubwa na nyama isiyo na ubora!, kuna siku huku Gongo la mboto asubuhi sana nimekuta carry inapakia ng'ombe aliyokufa.
 
Kuna jamaa yeye akishapima,anaweka kwenye mfuko ila kuna vipande anaacha kwenye mzani,usipokuwa makini anapita navyo
 
Back
Top Bottom