Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Simba imeruhusu bao 1 tu kwenye hatua ya makundi kwenye mechi 5 mpaka sasa na hakuna goli wamefungwa ndani ya boksi lao! Hali ni tofauti kidogo kwani katika makundi ya msimu juzi waliruhusu mabao 13 katika mechi 6.
Waliruhusu mabao hayo wakiwa na Wawa, Nyoni na Juuko Mourshid. Ni mabeki wabovu hawa!? Hapana. Hawa ni mabeki wazoefu na wenye uwezo mzuri wa kulinda ama kuzuia mashambulizi ya wapinzani iwe kwenye msitari au nje ya msitari.
Wawa kwa sasa yupo na Onyango Achieng, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni na Kennedy Juma. Je ni walinzi bora zaidi!? Nafikiri hapana. Nyoni hajarudi kwenye kiwango chake kile akicheza beki. Onyango ni beki mtulivu na makini ila Juuko hakuwahi kuwa rahisi.
Wawa ni kama amezaliwa upya katika kipindi ambacho hata wanasimba mwanzoni walikuwa na mashaka na beki zao namna zinavyocheza wakiona timu inaweza kuruhusu mabao mengi mengi kama msimu juzi ilivyokuwa.
Mabadiliko ya 4-3-3 na 4-4-2 kwenda kwenye 4-2-3-1 yameifanya Simba kukabia juu na kupunguza idadi ya wao kufikiwa kwenye safu yao ya ulinzi. Kupitia mfumo huu Simba imepunguza wachezaji wanaosimama juu kusubiri mpira ufike wautendee mambo yao.
Walikuwa na John Bocco, Emmanuel Okwi na Medie Kagere kama wachezaji wao kule mbele huku Clatous Chama, Jonas Mkude na James Kotei kimajukumu hapo hao watatu wa juu walikuwa wanausubiri mpira na Zimbwe na Nicolaus Gyan au Zana Coulibaly hawakuwa na wastani sawa wa kushambulia na kujilinda.
Ikafanya Simba kubaki na wachezaji watano tu wanaohusika moja kwa moja kwenye kujilinda. Kwa sasa wanakabia juu! Mugalu anawanyima nafasi mabeki wa timu pinzani kusogea juu kuiongezea nguvu timu yao huku Miquisone, Chama na Mkude au Mzamiru wakibaki kuvuruga dimba la kati. Taddeo akielemewa atacheza 'tough' au 'Rough' kisha Wawa atakuwa karibu kuondoa mpira huo vyema.
Atapiga pasi ndefu kwa madaha akijua wenzie wana usahihi wa matendo na hana papara kwa sababu krosi za wapinzani zinazuiwa na Zimbwe na Kapombe. Wameimarika sana. Hata ikipigwa mipira ya juu Onyango atacheza vyema kabisa.
Kazi ya Wawa kwa sasa ni rahisi kwa sababu ameimarika na wenzie ni bora. Manula yupo sawa sana pia.