Wawa mpya katikati ya Simba ile ile!

Wawa mpya katikati ya Simba ile ile!

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Simba imeruhusu bao 1 tu kwenye hatua ya makundi kwenye mechi 5 mpaka sasa na hakuna goli wamefungwa ndani ya boksi lao! Hali ni tofauti kidogo kwani katika makundi ya msimu juzi waliruhusu mabao 13 katika mechi 6.

Waliruhusu mabao hayo wakiwa na Wawa, Nyoni na Juuko Mourshid. Ni mabeki wabovu hawa!? Hapana. Hawa ni mabeki wazoefu na wenye uwezo mzuri wa kulinda ama kuzuia mashambulizi ya wapinzani iwe kwenye msitari au nje ya msitari.

Wawa kwa sasa yupo na Onyango Achieng, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni na Kennedy Juma. Je ni walinzi bora zaidi!? Nafikiri hapana. Nyoni hajarudi kwenye kiwango chake kile akicheza beki. Onyango ni beki mtulivu na makini ila Juuko hakuwahi kuwa rahisi.

Wawa ni kama amezaliwa upya katika kipindi ambacho hata wanasimba mwanzoni walikuwa na mashaka na beki zao namna zinavyocheza wakiona timu inaweza kuruhusu mabao mengi mengi kama msimu juzi ilivyokuwa.

Mabadiliko ya 4-3-3 na 4-4-2 kwenda kwenye 4-2-3-1 yameifanya Simba kukabia juu na kupunguza idadi ya wao kufikiwa kwenye safu yao ya ulinzi. Kupitia mfumo huu Simba imepunguza wachezaji wanaosimama juu kusubiri mpira ufike wautendee mambo yao.

Walikuwa na John Bocco, Emmanuel Okwi na Medie Kagere kama wachezaji wao kule mbele huku Clatous Chama, Jonas Mkude na James Kotei kimajukumu hapo hao watatu wa juu walikuwa wanausubiri mpira na Zimbwe na Nicolaus Gyan au Zana Coulibaly hawakuwa na wastani sawa wa kushambulia na kujilinda.

Ikafanya Simba kubaki na wachezaji watano tu wanaohusika moja kwa moja kwenye kujilinda. Kwa sasa wanakabia juu! Mugalu anawanyima nafasi mabeki wa timu pinzani kusogea juu kuiongezea nguvu timu yao huku Miquisone, Chama na Mkude au Mzamiru wakibaki kuvuruga dimba la kati. Taddeo akielemewa atacheza 'tough' au 'Rough' kisha Wawa atakuwa karibu kuondoa mpira huo vyema.

Atapiga pasi ndefu kwa madaha akijua wenzie wana usahihi wa matendo na hana papara kwa sababu krosi za wapinzani zinazuiwa na Zimbwe na Kapombe. Wameimarika sana. Hata ikipigwa mipira ya juu Onyango atacheza vyema kabisa.

Kazi ya Wawa kwa sasa ni rahisi kwa sababu ameimarika na wenzie ni bora. Manula yupo sawa sana pia.
1617710759883.jpg
 
Wawa bado ana mapungufu mengi sema team work inasaidia kuficha makosa yake kuna kipindi anatoa pasi boko kwa adui, anakaba kwa macho kwa kifupi ametufanyia kazi ya kutosha ni wakati wa kusema ahsante.
 
Acha ngebe. Vipi kuhusu Manula, Kapombe na Boko? Wote wameimarika zaidi wakiwa simba. Na bado azam wanatupatia dube msimu ujao
We ni kichaa? Hapa anazungumziwa wawa sio hao wengine
 
Yule Mzimbabwe Muduwha atakuja kuchukua nafasi ya Wawa, pia ni muda muafaka wa kumuachia Nyoni akapumzike, ana kipaji kikubwa sana, ni kiraka kila kona ila kasi na nguvu imeisha.
 
Wawa bado ana mapungufu mengi sema team work inasaidia kuficha makosa yake kuna kipindi anatoa pasi boko kwa adui, anakaba kwa macho kwa kifupi ametufanyia kazi ya kutosha ni wakati wa kusema ahsante
Duh aisee
 
Beki zetu zilionekana Uchochoro kwa kukosa Kiungo Mkabaji Asilia mwenye kiwango. Mambo mengi tunafanyiwa na LWANGA ingawa hatutaki kumpa heshima yake.

LWANGA ameziba pengo la Mkude na amefanya tuone Mkude kama Mtoto wa Kiwango cha UMISETA na sasa mabeki wetu akina WAWA na ONYANGO kazi imekuwa rahisi mnoo, lkn pia Great Saves za Manula ni Faida nyingine kwa Mabeki wetu.
 
Ubora wa Pascal Wawa umesababisha Peter Muduwa kuachwa Simba.
Jamaa anaachwa huku akiwa hajapewa nafasi ya kucheza hata mechi moja.

Source: African Sports today:
Simba SC have reportedly terminated the contract of Zimbabwean defender Peter Muduhwa just two months into his six months loan deal.
Muduhwa joined Simba SC on a six months loan from Highlanders FC after a fine outing in CHAN 2021 with his National Team Zimbabwe but has mutually terminated their relation after he failed to break into Simba SC CAF Champions League team.
 
Watakuwa wamefanya kosa kubwa, wawa umri umeenda, sasa hivi anaonekana bora kutokana na kazi anayofanya Lwanga na Onyango ila kama akibaki kama beki wa mwisho ni majanga hata mechi na vita alimwangalia foward akipiga mpira ambao Manura aliuokoa bila kufanya lolote
 
Labda Kocha anataka kumsajili yule Straika wa Mamelod, Ndio sababu wanapunguza idadi ya wachezaji wa kigeni. Kumbuka kuwa Simba bado ina idadi kubwa ya mabeki wa kati wanaolingana kwa ukaribu uwezo. Pia yule mshambuliaji mpya Mnigeria (Lokosa) nae ameingia mitini baada ya kukosa nafasi.

Simba kwa sasa imeshakuwa timu kubwa zaidi.
 
Bei ya wachezaji wa Mamelody si mchezo ni kubwa sana
 
Wala usiwe na shaka. Simba ipo chini ya tajiri, na mwakani itashiriki kombe la Dunia la vilabu baada ya kutwaa ubingwa wa Afrika mwaka huu.
Mamelody anauza wachezaji kwa mabilioni kuna wachezaji wazuri tunaweza kupata kwa bei chee kuliko kukimbilia mamelody
 
Wawa alikuwa Azam tu, huyu wa sasa bado hajafikia kiwango cha wawa wa Azam.
Mpaka akawafanya azam wakabeba club bingwa Africa, aisee alikuwa wa moto. [emoji23][emoji31][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom