Wawekezaji 30 kutoka Saudi Arabia wafanya ziara maalum nchini Tanzania

Wawekezaji 30 kutoka Saudi Arabia wafanya ziara maalum nchini Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
13 February 2025
Unguja Zanzibar,
Tanzania

Wawekezaji 30 kutoka Saudi Arabia wafanya ziara maalum nchini Tanzania - SADC

View: https://m.youtube.com/watch?v=M0oksDu6e44

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi mheshimiwa Dk Hussein Ali Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar bado ina fursa nyingi za uwekezaji katika sekta mbali mbali ikiwemo utalii, uchumi wa bluu, kilimo, mafuta na gesi pamoja na miundombinu.

Dk Hussein Ali Mwinyi aliyasema hayo mjini Zanzibar mara baada ya kuupokea ujumbe wa wawekezaji 30 kutoka Saudia Arabia waliofanya ziara maalum nchini humo kwa lengo la kutambua maeneo ya ushirikiano, uwekezaji na biashara.

Aidha mheshimiwa Rais Dr. Hussein Mwinyi alisema ziara hiyo itafungua ukurasa mpya wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
 
Back
Top Bottom