Wawekezaji (GSM & Mo Dewji) waheshimiwe!

Wawekezaji (GSM & Mo Dewji) waheshimiwe!

Dong Jin

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2018
Posts
968
Reaction score
2,034
Wawekezaji waheshimiwe !

Kupitia kampeni za 'NANI ZAIDI', Simba kuchangia pesa kujenga uwanja, Yanga kujiandikisha kidigigitali,, Picha halisi ni aina gani ya mashabiki waliopo kwenye vilabu vya Simba na Yanga imeonekana.

Katika zoezi la nchi nzima la kuchangisha pesa kujenga uwanja, ndani ya miezi (6) Simba SC walikusanya Tsh 60 Milioni !

Katika wiki moja tangu kampeni ya NANI ZAIDI izinduliwe, pesa zilizokusanywa nchi nzima hazitoshi hata kumnunua George Mpole !! Wakati kama mashabiki Milioni 1 tu kati ya watu Milioni (60) nchini wangetoa bukubuku klabu zingepata Tsh 1 BILIONI.

Halafu ukiwakuta mashabiki hao wanabishana vijiweni utasikia 'Mo Dewji, GSM watuachie timu zetu" wakati hata Tsh Mia mbovu hawachangii.

Safari moja tu ya Nigeria 🇳🇬 kwenda na kurudi kwenye Mchezo wa klabu bingwa Africa dhidi ya Rivers Utd GSM alitoa Tsh 700 Milioni including kukodi ndege Boing 787-8.

Safari moja ya kwenda mkoani kwenye mechi inagharimu si chini ya Tsh 250+ Milioni.

▪️ Hotel yenye hadhi ya nyota 4, 5.
▪️ Tiketi za ndege kwa watu si chini ya 30+ kwenda na kurudi.
▪️Chakula, Posho za mchezo nk..

Piga hesabu ndogo tu ni safari ngapi wamefanya kwa msimu ?!!!

Mishahara ya Wachezaji takribani (8) inaanzia Tsh 8 Milioni hadi Tsh 13 Milioni kwa kila mchezaji kwa mwezi mmoja, achilia mbali wanaolipwa Tsh Milioni 7, 6, 5 kwa mwezi nk.....

Kwa msimu GSM anatoa Tsh ngapi kwa mishahara tu including na wafanyakazi wengine wa klabu ?!!

Klabu ya Yanga inaishi moja ya kambi bora kabisa East Africa AVIC TOWN, kwa msimu GSM analipa Tsh 1+ BILIONI.

▪️Wamekodi nyumba 15
▪️Kila nyumba kodi (1+) Milioni
▪️Gharama za maji & Umeme.
▪️Gharama za Gym nk.....

Achilia mbali mamilioni ya pesa za usajili kuwaleta kina Djuma Shabani, Mayele, Bangala nk ....

Bajeti ya kuendesha klabu kwa msimu GSM anatoa takribani Tsh 6+ BILIONI.
.
.
Wapo watakaosema mbona anauza jezi ?!.... Ukitembea mtaani robo (3) ya jezi zilizovaliwa ni FEKI, It means pesa hiyo anaikosa.

Kama tunavyojuana Watanzania, mtu anaacha kununua jezi original ya Tsh 25 elfu anaenda kununua jezi feki ya Tsh 15 elfu bila kujua anaikosesha mapato timu yake na muwekezaji wake.

Inshort hawa matajiri waliowekeza kwenye vilabu vyetu 🇹🇿 WANAWEKEZA kwa mapenzi binafsi tu na timu na sio kwamba wanapata sana faida.

Kinachowavutia zaidi ni vitu (2)

1 - Wingi wa mashabiki

....Ambao wengi wao hawazisaidii timu, wao wanajua kulalamika tu timu ikifanya vibaya lakini ukiwaambia nendeni uwanjani hawaendi, jiandikisheni kidijitali hawajiandikishi, changieni uwanja Bunju, hawataki.

2 - Mapenzi binafsi na timu.

Wawekezaji waheshimiwe na walindwe 🙌

🔍 Tom Cruz
Screenshot_20220608-194438_1.jpg
 
Hizi tabia zetu maahabiki kupiga porojo zaidi ya vitendo zitasababisha wakati fulani hawa wawekezaji waanze kutupiga wakitengeneza faida, na sioni tatizo kwao kufanya hivyo, hakuna mfanyabiashara anayetaka biashara ya hasara, wote hutafuta faida.
 
Umesema kweli hizi timu mbili zina mashabiki wengilakini hawawezi kuziendesha timu hizi kwa pesa za mifukoni.Ukweli ni kwamba faida ya hawa matajiri ni ndogo sana kulinganisha na walivyotoa au wanavyosaidia,hatukatai kwamba hawafanyi biashara kwa hasara.Wote tuliona Yanga walivyotaabika kabla ya GSM na Simba kabla ya Mo.Muhimu mifumo yenye tija ibadilike tu jinsi ya kuendesha hizi klabu zisiwe tegemezi
 
M700[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yes! Piga hesabu... Mtu mmoja kusafiri na kulala hoteli ya hadhi ya nyota 5 kwa muda wa siku si chini ya 3, plus chakula na huduma nyinginezo pamoja na sehemu ya kufanyia mazoezi.... Hapo bado hujaongeza gharama za kuitoa timu kambini mpaka uwanjani na kurudi tena!

Hiyo ni kwa mtu mmoja.... Pigia hesabu kikosi kizima cha wachezaji 24+, benchi la ufundi, maafisa waandamizi, nk, nk, nk.....

Tusijisahaulishe kilichowakuta biashara.....

NB: wawekezaji wapewe heshima wanayostahili
 
Umesema kweli hizi timu mbili zina mashabiki wengilakini hawawezi kuziendesha timu hizi kwa pesa za mifukoni.Ukweli ni kwamba faida ya hawa matajiri ni ndogo sana kulinganisha na walivyotoa au wanavyosaidia,hatukatai kwamba hawafanyi biashara kwa hasara.Wote tuliona Yanga walivyotaabika kabla ya GSM na Simba kabla ya Mo.Muhimu mifumo yenye tija ibadilike tu jinsi ya kuendesha hizi klabu zisiwe tegemezi
Of course, 👍
 
Aliwahi sema pia Mo kua anatoa hela kwa mapenz tu na Simba hapati faida washabiki uchwara wasiojua hesabu wanavyodhani ,,Ni vile anaipenda simba..Hawa jamaa waheshimiwe aisee kuendesha timu sio mchezo,,mtu familia ya mke na mtoto inamshinda anasema eti tuachie timu [emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom