Yote hayo nakubali,yaani kwa takwimu zinaonesha mashabiki hawana uwezo hata kidogo,
Nakubaliana.
Mo Dewji aliwahi kunukuliwa kuwa anatumia zaidi ya bilioni 4,kwa Kila msimu, na ukiangalia ni kweli,
Mapato ya uwanja,Kodi za majengo ya pale Msimbazi,hata hizo hela walizopata Simba pindi wanafika hatua ya makundi na robo final,bado ukiipigia hesabu,
Ukaigawanya kotekote, hakuna kitu tajiri anapata
Maswali ya kujiuliza,
Je, inawezekanaje mtu aiongoze taasisi kubwa kabisa,pasipo kupata faida?
Nini kipo nyuma,juu ya huu uwekezaji,ukitazama kwa macho mawili,jibu ni mapenzi kwa timu lakini,jicho la tatu linakataa,kutokana na aina ya matajiri tulionao,
Vibarua tu wananyanyaswa huko kwenye viwanda vyao kwa ujira mdogo,
Huku wao Wanatoa,pesa nyingi pasi na faida
Lazima Kuna namna, either kusafisha pesa haramu,kutoka kundi fulani Tena si mtu mmoja.
Au kutengeneza pesa zaidi kwa njia za kilaghai,huku hayo mambo yakifanywa na vigogo wa nchi kwa mgongo wa Hawa matajiri.