Nimeamini mpira wa bongo bado sana, wanaohangaika ni mashabiki na wala sio viongozi..
Kuna weekend moja zimepita siku kadhaa, ilkua siku ya jumamosi, Simba SC ilikua na mechi kubwa tu nje ya nchi.
Nilikuwa napunga upepo maeneo ya Oyersterbay kwenye hotel moja majira ya jioni, muda ambao Simba sc ilkua inacheza mechi yake, mwekezaji Mo Dewji na yeye alikuwepo hapo pamoja na rafiki yake mmoja hakua na mpango wa kuangalia mechi.
Siwezi kusema nini alkua anafanya ila alikua haangalii mpira na mpira ulkua hauoneshwi, mashabiki ndio mnaoangaika, viongozi hua mpango hawana ndio kwanza alikua kaagiza chakula.