Wawekezaji hawavutiwi kwa kusafiri

Wawekezaji hawavutiwi kwa kusafiri

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,932
Reaction score
13,306
Rais wa zamani wa Zaire (sasa Congo) Mobutu Seseseko alisafiri kwenda Ulaya, Marekani na Asia zaidi ya mara 890 kwa muda wote aliokaa madarakani kwa miaka 32, lakini hiyo haikuwafanya wawekezaji wavutiwe kuwekeza Congo.

Si tu kwamba alisafiri na kila aina ya mbwembwe bali alikutana nao na kuzungumza nao na kuwasihi waende nchini kwake kuwekeza.
Miaka yote 32 ya Mobutu madarakani,hakupata hata mwekezaji mmoja wa maana.

Kinachowavutia wawekezaji ktk Taifa lolote Duniani, siyo Rais kusafiri,bali hali ya mazingira ya nchi, hasa Utawala Bora (Demeanor) kuheshimu haki za Binadamu, Demokrasia na Uhuru wa vyombo vya Habari.

Wawekezaji wapo ktk namna Tofauti, kuna wengine wanatamani kuwekeza ktk vyombo vya Habari,sasa makampuni yao yataandikaje Habari kwenye Taifa ambalo halina Uhuru wa Habari?

Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Upinzani Serikali inamtuhumu kuwa Gaidi?

Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo Rais wake anakiri hadharani kuwa kiongozi wa Upinzani ni Gaidi? Rais anadai kuwa kiongozi wa Upinzani ni Gaidi huku kesi ikiwa Mahakamani bado.

Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo watu wanaoikosoa Serikali wanapigwa risasi hadharani na wengine kupotea kama shilingi chooni?

Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo maiti zinaokotwa kwenye viroba,mitoni na Baharini, halafu Serikali inajibu kwamba hao ni wakimbizi tu walifia kwenye magari ya mizigo, sasa na Baharini walifikaje? Na mlijuaje kuwa ni wakimbizi?

Na Intelligence yenu ilishindwa vp kuwapata waliowatupa mitoni na Baharini.

Na wakati huo huo kuna waliopotea kwa kukosoa Serikali?

Wawekezaji huvutiwa na Taifa lililostaarabika na siyo blabla kila siku miaka 50 yote blabla tu.

Wawekezaji watakuja vp kuwekeza ktk Taifa ambalo hata Tajiri mwenzao anatekwa na watu wa nje kisha watekaji wote wanatoweka baada ya kumtupa waliyemteka katikati ya jiji na kisha kuvuka mpaka na kuyeyuka?

Wawekezaji watakuja vp kuwekeza kwenye Taifa ambalo Kodi ni kubwa hadi kwa maskini wa kutupwa?

Mtapiga sana kelele na mtaishia kuwatazama wawekezaji kwenye TV tu.
 
Umeandika uzi mrefu wa malalamiko. Mazingira ya Mobutu ni ya miaka ile ya uhuru, ambayo hayafanani kabisa na ya sasa hivi.

Nina uhakika tangu rais wa awamu hii aingie ikulu hujasikia tena habari ya watu kuokotwa wakiwa ndani ya viroba pale coco beach, usikariri maisha kwamba jana lazima ifanane na leo hii.

Unachekesha sana, unaleta akili zile zile za unazi na ushabiki wa Simba na Yanga kwamba wanachekana baada ya mmoja kufungwa huko nje. Unaiombea mabaya Tanzania ambayo unatembea na passport yake mfukoni, nje na ndani ya nchi.
 
Ni kujizuzua tu

 
Umeandika uzi mrefu wa malalamiko. Mazingira ya Mobutu ni ya miaka ile ya uhuru, ambayo hayafanani kabisa na ya sasa hivi...
ifike wakati uazime hata akili kidogo, wewe ni mmoja ya watu wajinga kabisa kuwahi kutokea chini ya jua.

Yaani wewe hutaki kusikia Serikali ya CCM inakosolewa, CCM ndo mungu wenu nyie watu mambumbumbu wa kutupwa.

Unakiri kumbe watu kuokotwa kwenye viroba wakati wa Magufuli, lakini wakati huo huo ulitetea Serikali hiyo katili kwa nguvu zako zote.
Sasa hivi tena unamtetea mama Tozo kwa kushiriki kumbambikia Mbowe kesi ya uongo.

Wewe ni zaidi ya mwanamke malaya, pathetic huna akili kabisa wewe.

Hata mada hujaielewa unakimbilia mihemko ya ki CCM,una ubongo wenye funza wewe si bure
 
Umeandika uzi mrefu wa malalamiko. Mazingira ya Mobutu ni ya miaka ile ya uhuru, ambayo hayafanani kabisa na ya sasa hivi...
Kusikia au kutosikia Jambo fulani ni uamuzi wako.

Unasema tangu awamu hii iingie hatujasikia maiti zikiokotwa coco beach, kwani ni lazima iwe coco beach?

Sasa hivi wanatupwa msituni kisarawe, hii hapa habari ya kilichotokea September mwaka huu.

Screenshot_20211207-131627_1.jpg
 
The hate is so much,

You can easily see it from the writing, this makes your argument void.

Kind regards
 
Kama wawekezaji wanapenda rais anaesafiri basi Tanzania ingekua zaidi ya Ney York kwa enzi wa Kikwete maana ilikua ni safari juu ya safari.
 
Umeandika uzi mrefu wa malalamiko. Mazingira ya Mobutu ni ya miaka ile ya uhuru, ambayo hayafanani kabisa na ya sasa hivi...
Pamoja na hayo.

Kuna hoja ameongea hapa za msingi sana.

Hawa watu wangeacha kushupaza shingo.

Waweke mambo sawa kwa maslahi ya nchi tatizo ni kwamba wanaangalia maslahi binafsi na hawajali kuhusu wengine
 
Rais wa zamani wa Zaire (sasa Congo) Mobutu Seseseko alisafiri kwenda Ulaya, Marekani na Asia zaidi ya mara 890 kwa muda wote aliokaa madarakani kwa miaka 32, lakini hiyo haikuwafanya wawekezaji wavutiwe kuwekeza Congo...
Wewe tukuza boli mobutu hakutembea kwa kutafuta wafadhili alikuwa anatembea kustarehe tu

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
ifike wakati uazime hata akili kidogo, wewe ni mmoja ya watu wajinga kabisa kuwahi kutokea chini ya jua...
Mwanamke malaya ni wewe usio na msimamo kichwani kwako, mwepesi wa kukimbilia matusi badala ya kujenga hoja.

Unazeeka unalalama kama mja mzito. Kuikosoa serikali hakuna anayeweza kupinga wala kuzuia ni haki yako.

Jenga hoja zilizoshiba uone kama utakosolewa.
 
Rais wa zamani wa Zaire (sasa Congo) Mobutu Seseseko alisafiri kwenda Ulaya, Marekani na Asia zaidi ya mara 890 kwa muda wote aliokaa madarakani kwa miaka 32, lakini hiyo haikuwafanya wawekezaji wavutiwe kuwekeza Congo...
Masuala ya kodi hayakwepeki lakini yanazungumzika. Na awamu ya sita ilichokiweza na kujishusha, kutambua kuwa wao ni binadamu wenye kupaswa kushuka chini wanapokuwa katika mijadala ya kuwavutia wawekezaji.

Naamini Mama Samia amewaleta wawekezaji wengi na atazidi kuwalete, kuna suala la covid19 amelishughulikia kimataifa na ameonyesha kujali.
 
Tanzania ya serikali ya CCM ni kichwa cha mwendawazimu kinachotembea.

Imagine Rais punguani kama huyo atang'ang'ania kuongoza miaka kumi.

Yaani urais kwake ni sifa wala siyo majukumu yenye tija.
 
Masuala ya kodi hayakwepeki lakini yanazungumzika. Na awamu ya sita ilichokiweza na kujishusha, kutambua kuwa wao ni binadamu wenye kupaswa kushuka chini wanapokuwa katika mijadala ya kuwavutia wawekezaji.

Naamini Mama Samia amewaleta wawekezaji wengi na atazidi kuwalete, kuna suala la covid19 amelishughulikia kimataifa na ameonyesha kujali.
Wawekezaji gani wameletwa hadi sasa?
 
Back
Top Bottom