My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,306
Rais wa zamani wa Zaire (sasa Congo) Mobutu Seseseko alisafiri kwenda Ulaya, Marekani na Asia zaidi ya mara 890 kwa muda wote aliokaa madarakani kwa miaka 32, lakini hiyo haikuwafanya wawekezaji wavutiwe kuwekeza Congo.
Si tu kwamba alisafiri na kila aina ya mbwembwe bali alikutana nao na kuzungumza nao na kuwasihi waende nchini kwake kuwekeza.
Miaka yote 32 ya Mobutu madarakani,hakupata hata mwekezaji mmoja wa maana.
Kinachowavutia wawekezaji ktk Taifa lolote Duniani, siyo Rais kusafiri,bali hali ya mazingira ya nchi, hasa Utawala Bora (Demeanor) kuheshimu haki za Binadamu, Demokrasia na Uhuru wa vyombo vya Habari.
Wawekezaji wapo ktk namna Tofauti, kuna wengine wanatamani kuwekeza ktk vyombo vya Habari,sasa makampuni yao yataandikaje Habari kwenye Taifa ambalo halina Uhuru wa Habari?
Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Upinzani Serikali inamtuhumu kuwa Gaidi?
Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo Rais wake anakiri hadharani kuwa kiongozi wa Upinzani ni Gaidi? Rais anadai kuwa kiongozi wa Upinzani ni Gaidi huku kesi ikiwa Mahakamani bado.
Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo watu wanaoikosoa Serikali wanapigwa risasi hadharani na wengine kupotea kama shilingi chooni?
Au watafunguaje viwanda kwenye Taifa ambalo maiti zinaokotwa kwenye viroba,mitoni na Baharini, halafu Serikali inajibu kwamba hao ni wakimbizi tu walifia kwenye magari ya mizigo, sasa na Baharini walifikaje? Na mlijuaje kuwa ni wakimbizi?
Na Intelligence yenu ilishindwa vp kuwapata waliowatupa mitoni na Baharini.
Na wakati huo huo kuna waliopotea kwa kukosoa Serikali?
Wawekezaji huvutiwa na Taifa lililostaarabika na siyo blabla kila siku miaka 50 yote blabla tu.
Wawekezaji watakuja vp kuwekeza ktk Taifa ambalo hata Tajiri mwenzao anatekwa na watu wa nje kisha watekaji wote wanatoweka baada ya kumtupa waliyemteka katikati ya jiji na kisha kuvuka mpaka na kuyeyuka?
Wawekezaji watakuja vp kuwekeza kwenye Taifa ambalo Kodi ni kubwa hadi kwa maskini wa kutupwa?
Mtapiga sana kelele na mtaishia kuwatazama wawekezaji kwenye TV tu.