Wawekezaji Sekta ya Mifugo

Mkuu hawa bata bukini na mallad naweza pata mayai nitotoleshe? Also, unaweza nipa contact za jamaa yako wa Handeni juu ya mbuzi? Natanguliza shukrani
 
Mkuu hawa bata bukini na mallad naweza pata mayai nitotoleshe? Also, unaweza nipa contact za jamaa yako wa Handeni juu ya mbuzi? Natanguliza shukrani
Salaam nisamehe kuchelewa kukujibu naomba unitafute in box kaka nitakupa mawasiliano usijali na kama upo Dar karibu sana nyumbani uone baadhi ya mradi wangu tuweze badilishana mawazo ktk ufugaji, kuhusu mayai nisinge kushauri uchukuwe mayai, nakushauri nunuwa Bata kabisa watagie kwako ndio utotoleshe.
 
Kumbe mbuzi wanauzwa ghali hivi, nmezoea wa mnadani 50-100
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. jamani mvua hizi tuwe waangalifu na mifugo yetu, kwa bata na kuku typhoid tuwakinge. Kwa Mbuzi na Ngombe foot and mouth na minyoo tuwe waangalifu navyo tafadhalini sana. Mbarikiwe nyote.
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. jamani mvua hizi tuwe waangalifu na mifugo yetu, kwa bata na kuku typhoid tuwakinge. Kwa Mbuzi na Ngombe foot and mouth na minyoo tuwe waangalifu navyo tafadhalini sana. Mbarikiwe nyote.
Amen mtumishi wa Mungu
 
Kumbe mbuzi wanauzwa ghali hivi, nmezoea wa mnadani 50-100
Ni kweli hasa unapo hitaji hizo mbegu kwaajili ya ufugaji ni bei kubwa sana, ila mimi ningeshauri sana mtu kabla ya kuanza kuingiza mbegu ktk zizi lako tafadhali tutembelee sisi tulio anaza kufuga ujifunze kwanza halafu ndio uchukuwe jukumu la kununua mbegu za kuzalisha sasa.
Nashukuru sana kuna mmoja wetu humu alifika nyumbani na tulibadilishana mawazo vyema na naamini alijifunza kitu, karibuni sana ktk ufugaji na tujijengee himaya nzuri ya wafugaji, mbarikiwe nyote.
 
Masai na wasukuma ila wapo porini sana wanang'ombe mpaka 1000
 
Mkuu akilishwa viagra au vumbi ya kongo hawezi perform vizuri. Madawa mengi ya binadamu ndio hayo hayo ya wanyama.Nakumbuka wakati nafuga nilikuwa naanywesha kuku wangu anti biotics(rangi mbili).
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu , naomba niwakumbushe kitu kimoja tafadhalini. Kipindi hiki cha mvua hali inakuwa sio nzuri kabisa kwa mifugo yetu magonjwa yana kuwa mengi, na hiki ndio kipindi cha Mbuzi kupata ugonjwa wa homa ya mapafu wataalamu wanatusisitiza kuchoma chanjo ya CCPP kwaajili ya homa ya mapafu ambayo inamaliza mbuzi haraka sana, mimi wakwangu nimeawadunga juzi wote hapo ni mpaka mwakani tena.
Kwa sasa nakuwa nawatibu minyoo na mafua maana hiki ni kipindi cha magonjwa hayo. Kuhusu chanjo ya Mouth nitaleta mrejesho wake pia maana nawasubiri ma Vet wanipatie mwongozo. Niwatakieni siku njema Mbarikiwe sana.
 
Habari Mtumishi!
Mimi nipo huku Mtwara, Je ninaweza kufuga mbegu ya Galla?
 
Habari Mtumishi!
Mimi nipo huku Mtwara, Je ninaweza kufuga mbegu ya Galla?
Ama hakika unaweza, Galla ni mbuzi waweza mfuga mahala popote kumbuka Galla ni mbuzi aliye tayarishwa kwaajili ya sehemu kame na anahimili magonjwa kuliko mbuzi mwingine yoyote, mfno hapa kwangu nahizi mvua mbuzi nyingi zizhzrisha kwaajili ya haya majani mabichi lakini wao wanadunda bila ya shida, ningekushauri kama upo tayari nitakupatia number ya msambazaji wa Galla mimi nitakupokealea hapa dar basi watafika kwako mtwara. Na ningekushauri kama utakuja Dar njoo nyumbani kwangu uangalie kwanza tunavyo fuga na uwaone Galla ndipo ukate shauri la kuwaagiza toka arusha.
 
Nashkuru sana mtumishi, kwa sasa hivi nipo kwenye ujenzi wa mabanda ya kawaida tu, nikiwa tayari by december nitafika nyumbani nijifunze kwa uhalisia zaidi.
 
Nashkuru sana mtumishi, kwa sasa hivi nipo kwenye ujenzi wa mabanda ya kawaida tu, nikiwa tayari by december nitafika nyumbani nijifunze kwa uhalisia zaidi.
Karibu sana ningekushauri kitu kwenye mabanda,jitahidi uweze kuachanisha vizuri hapo chini ili wasiumize miguu wakati wa kulala maana Mbuzi madume wao huanza fujo kwenye kuminamoja alfajiri, hapo huwa mbuzi wana vunjika sana miguu upana kati ya mbao na mbao ukiwa mkubwa sana, uanagalie upuepo unapo tokea ili usiweke madirisha makubwa sana upepo mwingi huwasumbuwa wakati wa usiku wanapo lala.
Utengeneze banda la pemebenikwaajili ya wajukuu kupumzika hasa wakati wa mama wamaekwenda malishoni.uweke sehemu itakayo kuwa rahisi kutoa samadi kila utakapo kusafisha banda maana nijambo la umuhimu sana ktkl malezi ya mbuzi.
 
Hee!
Kumbe hadi mabanda yana utaalamu wake.

Mm niliwaza kusimisha banda ya mgongo wa tembo lenye uwazi wa wavu kwa juu.

Kisha niwarundike humo.

Nadhani natakiwa kujifunza vingi zaidi katika hii Project.
 
Hee!
Kumbe hadi mabanda yana utaalamu wake.

Mm niliwaza kusimisha banda ya mgongo wa tembo lenye uwazi wa wavu kwa juu.

Kisha niwarundike humo.

Nadhani natakiwa kujivunza vingi zaidi katika hii Project.

..banda lako linatakiwa liwe kama kichanja, liwe na uwazi chini.

..unaweza kujifunza toka kwa huyo mtaalamu hapo chini.

 
Kwakweli nimehamasika na hawa mbuzi aina ya Galla natamani kuona walivyo nami niagize pls mwenye mawasiliano tafadhali pm
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…