Ottician
Senior Member
- Jul 6, 2019
- 103
- 81
- Thread starter
-
- #61
Kwa mahali nilipo, kondoo wanalika na nyama yake inapendwa. Cha muhimu nachojifunza kwenye ufugaji wa kondoo kama utaamua kujikita hakikisha uwe na breed bora kwa ajili ya nyama, mfano dorper- hawa unaweza chinja kuanzia miezi sita na uzito wa nyama ukapata 16-20.Kondoo hawana mambo mengi, changamoto kubwa ni minyoo ( hakikisha unajipanga kupambana na hili). Kuna breed zingine kama meat master kutoka South Africa pia ni nzuri. Local breed kama Red maasai ukuaji sio wa haraka,inahitaji muda japo ni wagumu na wavumilivu kwa hali zetu.
Waturuki wanapenda sana kondoo kwa waliokwisha fanya biashara nao wanalielewa hilo, wanalipa kwa ubora.Pia soko sio ndani tu, ukijikita vizuri unasafirisha nyama packed ( tujaribu fikiria kwa upana huu).
Binafsi natafuta ardhi mkoa wa shamba nianze kuliendeleza kidogo kidogo ( investment ya miaka mbele) kwa ajili ya kondoo. Nikihitaji Red maasai, Dorper, Nairobi meat master basi Jirani zetu Kenya wako vizuri kwa breeding ( wametutangulia kiu kweli)