Wawekezaji Sekta ya Mifugo

Wawekezaji Sekta ya Mifugo

Kwa mahali nilipo, kondoo wanalika na nyama yake inapendwa. Cha muhimu nachojifunza kwenye ufugaji wa kondoo kama utaamua kujikita hakikisha uwe na breed bora kwa ajili ya nyama, mfano dorper- hawa unaweza chinja kuanzia miezi sita na uzito wa nyama ukapata 16-20.Kondoo hawana mambo mengi, changamoto kubwa ni minyoo ( hakikisha unajipanga kupambana na hili). Kuna breed zingine kama meat master kutoka South Africa pia ni nzuri. Local breed kama Red maasai ukuaji sio wa haraka,inahitaji muda japo ni wagumu na wavumilivu kwa hali zetu.
Waturuki wanapenda sana kondoo kwa waliokwisha fanya biashara nao wanalielewa hilo, wanalipa kwa ubora.Pia soko sio ndani tu, ukijikita vizuri unasafirisha nyama packed ( tujaribu fikiria kwa upana huu).

Binafsi natafuta ardhi mkoa wa shamba nianze kuliendeleza kidogo kidogo ( investment ya miaka mbele) kwa ajili ya kondoo. Nikihitaji Red maasai, Dorper, Nairobi meat master basi Jirani zetu Kenya wako vizuri kwa breeding ( wametutangulia kiu kweli)
 
Ama hakika unaweza, Galla ni mbuzi waweza mfuga mahala popote kumbuka Galla ni mbuzi aliye tayarishwa kwaajili ya sehemu kame na anahimili magonjwa kuliko mbuzi mwingine yoyote, mfno hapa kwangu nahizi mvua mbuzi nyingi zizhzrisha kwaajili ya haya majani mabichi lakini wao wanadunda bila ya shida, ningekushauri kama upo tayari nitakupatia number ya msambazaji wa Galla mimi nitakupokealea hapa dar basi watafika kwako mtwara. Na ningekushauri kama utakuja Dar njoo nyumbani kwangu uangalie kwanza tunavyo fuga na uwaone Galla ndipo ukate shauri la kuwaagiza toka arusha.
Ni kweli kabisa. Niliwahi kuwapoteza mbuzi karibia wote kwa homa ya mapafu 2018. Nikabakiwa na Galla 2 na chotara mmoja. Wote ni wazaa mapacha karibia kila uzao. Mbegu tamu sana.
 
Kinacho kwamisha wengi ktk mradi wa Mbuzi ni maeneo kwaajili ya malisho, mbuzi ukitaka waende vyema unapashwa kuwachunga ktk free zone watamea vyema sana.
Nina heka kama 300bhuko kusini hapo naweza kufunga mbuzi wangapi?
 
Nadhani wanaofuga wanayajua masoko
Mama D kwakweli soko bado liko chini sema shida hao Galla/Isiolo wa sh Laki 3 mara Nyingi unapotafuta Mbegu ndio bei zinakuwa kubwa hivyo ila soko ndio mapambano sasa,
 
Mama D kwakweli soko bado liko chini sema shida hao Galla/Isiolo wa sh Laki 3 mara Nyingi unapotafuta Mbegu ndio bei zinakuwa kubwa hivyo ila soko ndio mapambano sasa,
Vipi ukienda kama mnunuzi wa kawaida
 
Back
Top Bottom