Wawekezaji wahusiwa kutumia Sayansi, tafiti na ubora wa vifaranga ufugaji samaki

Wawekezaji wahusiwa kutumia Sayansi, tafiti na ubora wa vifaranga ufugaji samaki

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
126
Reaction score
201
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kuwahamasisha wawekezaji katika sekta ya uvuvi kuzingatia matumizi sahihi ya Sayansi na Tafiti za uvuvi katika kusimamia ubora na uzalishaji wa vifaranga vya samaki ili kuwa na tija katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba..

Kauli ya Serikali imetolewa Agosti 10, 2026 na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa wakati wa ziara yake mkoani Mwanza kwenye Shamba la Ufugaji Samaki kwa Njia ya Vizimba la Big Best Company Limited lililopo Ilemela mkoani humo.

Soma zaidi: Vifaranga Vya Samaki Milioni 1.5 Vyapandikizwa Ziwa Rwakajunju - Karagwe

Alieleza kuwa serikali kupitia wizara anayoisimamia inaendelea kuwahamasisha wawekezaji wakubwa katika sekta ya uvuvi kuchangamkia fursa ya kuwekeza katika viwanda vya chakula cha samaki huku na akasisitiza juu ya matumizi ya Sayansi, tafiti pamoja na vifaranga vyenye ubora katika ufugaji wa samaki.

Kwa upande wake, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya 'The Big Best Company Limited', Prof. Samwel Mchele Limbu amesema shamba hilo linauwezo wa kuzalisha vifaranga vya samaki milioni 8 na kwamba kampuni hiyo yenye thamani ya shilingi Bilioni 205 ina vizimba 250 vya kulelea samaki, vizimba 500 vya kuvunia samaki na tayari ipo kwenye mpango wa ujenzi wa Kiwanda chenye uwezo wa kuzalisha tani 72,000 za chakula cha samaki kwa mwaka mkoani Mwanza.



Source: Clouds Media
 
Back
Top Bottom