Wawekezaji wanaweza angalia na zao la Sugar Beet

Masamila

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2014
Posts
6,490
Reaction score
7,422
Kwa kweli bei ya sukari hapa TZ sio fair kweli mtu tununue kg kwa zaidi ya dola moja ya kimarekani na ukizingatia nchi yetu ilivyo na utajiri wa ardhi kubwa na mvua maeneo yote

Anyway dodoso kuhusu fursa zao la Sugar beet, hili zao linastawi nyanda za juu kwenye baridi na milimani milimani huko. Kinachonivutia hasa katika zao hili ni jinsi linavyozaa sana kuliko miwa ambayo tunaitegemea kuzalisha sukari yetu.

Zao hili linazaa sana na mavuno yake ni zaidi ya tani 20 kwa ekari moja. Tuna maeneo mengi sana yamebaki kutumika kuzalishia mkaa tu yangelimwa hili zao

Zao hili linazalisha sukari kuliko miwa (miwa ni asilimia 10 hadi 15 za muwa unaoingizwa kuchakatwa kuishia kuwa sukari wakati zao hili ni kuanzia asilimia 13 hadi 18)

Maeneo ya nyanda za juu kusini , kanda ya kaskazini umasikini haukutakiwa kuwepo kabisa.

 
Kama utakubaliana nami hilo zao ni mojawapo ya mazao ya kwanza kabisa yaliyotumika kuzalisha sukari kihistoria.

Swali. Ni kwa nini halikupewa umuhimu kuliko zao la miwa?

Swali la pili. Kuotesha zao ni jambo moja na kuchakata upate sukari ni jambo lingine ikiwa kweli umedhamiria kuondoa uhaba wa sukari.

Je tunayo teknolojia ya kuchakata tupate hiyo sukari kwa kiwango ambacho kitaondoa au kupunguza tatizo?

Ila kama umeamua kulima mboga mboga aina hiyo hapo naweza kukuelewa
 
Kuhusu asilimia ulizozungumzia sijakupata. Na hata ukipima wingi wa sukari utakayopata kwenye mua na hilo zao inahitaji comperative study maana sikuhizi kuna varieties ambazo ni maalumu kwa utengenezaji wa sukari.
 
Hilo la sugar beets nimeligusia kwenye baadhi ya mada humu ila naona wengi hawalifahamu ila kama wangehamasisha watu kama SUA na kufanya majaribio kwa kweli lingesaidia sana
Kwa mfano Ulaya wanalima sana baada ya kuona miwa waliohamasisha huko Brazil na nchi za karibu Yao ikawa mbali sana na kupata mbadala wa sugar beets
 
Maeneo ya miwa yangelimwa mpunga sababu soko la mpunga liko jirani sana (nchi majirani wote wanatutegemea kwenye mchele)

Nchi za Ulaya na Marekani wanalilima hili zao (Sugar beet) kwa ajili ya sukari ,hawajakaa wategemee tu muwa ambao haukubali kwenye nchi zao

Kuhusu tech: hapa ni mwekezaji ananunua tu mitambo ,India na China wanatengeneza na kuuza sana mitambo ya viwanda
 
Kuhusu asilimia ulizozungumzia sijakupata. Na hata ukipima wingi wa sukari utakayopata kwenye mua na hilo zao inahitaji comperative study maana sikuhizi kuna varieties ambazo ni maalumu kwa utengenezaji wa sukari.
Ule muwa ukiingizwa kwenye uchakataji asilimia yake 10 hadi 15 ndio inakuwa sukari
 
Nimekupata vizuri mkuu. Kenya vipi utafiti wao. Je ulifanikiwa?
 
Nimekupata vizuri mkuu. Kenya vipi utafiti wao. Je ulifanikiwa?
Afrika kwa uzembe hatuchekani

Nikicheki geography yao (Kenya) kwenye ramani hili zao wanastawisha tu
 
Mkuu tuelezee na soko lake kwa ujumla.Je, ni lazima kulichakata ndo uuze au unaweza uza hata likiwa shambani?


Soko limelindwa na serikali kwa kuzuia uingizaji wa sukari kutoka nje ya nchi

Ukishavuna kama una mtaji mkubwa kuna mashine/mitambo ya kuchakata ili kutengeneza sukari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…