Nominee
JF-Expert Member
- Sep 5, 2017
- 464
- 1,260
Habarini wakuu.Maisha yana funzo kubwa sana,ukiwa na roho nyepesi waweza kukata tamaa.
Ilikuwa ni siku ya jumamosi asubuhi,mwezi wa kumi mwaka 2019,miezi miwili tangu nihitimu shahada yangu ya kwanza kutoka chuo kikuu cha Dodoma(UDOM).Nipo zangu nimejipumzisha ndani ya chumba nilichopanga maeneo ya "Makulu" kwa kuwa sikutaka kurudi mkoani nilipozaliwa.Ghafla simu yangu ya mkononi ikaanza kuita,mpigaji ni mpenzi wangu tuliesoma pamoja chuoni.Nikaipokea haraka na kuiweka sikioni,'Mungu wangu!!..Nikasikia mtu analia kwa uchungu huku akivuta mafua kwa sekunde kadhaa.Niliingiwa na uwoga ila nikajikaza na kumuuliza kipi kinamfanya alie?.Ndipo aliponieleza kuwa amefukuzwa kwao baada ya kugundulika ni mjamzito na huo ujauzito ni wa kwangu,
Sikuonesha kushtuka ingawa moyoni nilikuwa na hofu kuu.Mimi mwenyewe nalalia kagodoro kadogo nilikonunua kwa msaada wa bum.Sina kitanda wala vyombo vya kupikia,sina meza wala kiti cha kukalia.Sina kazi ya kueleweka niseme nitajivunia.Kwahiyo sikuwa na hela kusema nitamtumia.Na hapo aliponipigia alikuwa tu porini,mbali kidogo na kijijini kwao.
Nikamfariji kwa kumwambia anyamaze,asilie bali anitumie namba za wazazi wake nijaribu kuwabembeleza.Alinitumia nami nikawapigia muda huohuo,alipokea baba.Kwanza nikawasalimu na kukiri kosa kuwa ni kweli mimi na mtoto wao tuliteleza tukafanya uzinzi uliosababisha ujauzito ule,kwahiyo watusamehe na wasimfukuze binti yao.Mimi nimekiri ujauzito ni wa kwangu na nitajitahidi kutoa matunzo...Daah hawakunielewa,yani nikawa kama nimechochea moto badala ya kuuzima.Baba yake alinishambulia sana kwa maneno ya kejeli na vitisho na kusema hataki kufuga makahaba.Basi ilinibidi nikate tu simu,hakuna namna.
Nikampigia tena simu mpenzi wangu,nikamueleza jinsi nilivyoongea na wazazi wake.Nikamshauri aende hata kwa majirani au ndugu zake wengine,wanaweza kumsaidia na kwenda kumuombea msamaha.Alikubali na kuelekea kwa shangazi yake ambae anaishi karibu na kwao.Siku ya pili walitanguzana hadi kwao kuomba msamaha ila baba yake bado alikataa na alimtishia kuwa asimuone tena pale kijijini,la sivyo anaweza hata kumuua eti kisa amemtia aibu.Basi ilibidi waondoke.
Baada ya siku mbili niliuza simu janja yangu(Smart phone) kwa elfu 80 Kisha nikamtumia nauli ya kuja Dodoma nilipo kutoka huko kwao(MWANZA).Nilishajua maisha yatazidi kuwa magumu akija huku nilipo ila sikuwa na namna.Nikajipa moyo "NITAPAMBANA".
Hatimae akaingia Dodoma rasmi na ujauzito wake wa miezi karibia mitatu kasoro.Nikampokea kwa mikono miwili na kuyaanza rasmi maisha ya mke na mume.
Kitaaluma mimi ni mwalimu,na kuna shule binafsi ya sekondari nilikuwa nafundisha kwa mshahara wa laki moja kwa mwezi.Ni mshahara mdogo sana kwa maisha ya Dodoma.Kodi ya chumba ni elfu 25 kwa mwezi(Nyumba ina umeme ila haina maji),bado bili ya umeme,na hela ya kula.
Mungu alivyo wa ajabu,siku nne tu baada ya mke wangu kuja nikasimamishwa kazi kwa madai kwamba shule haina uwezo wa kuendelea kunilipa.Nilijitahidi kutafuta shule nyingine lakini nilikosa nafasi.
Ikanipasa nitafute kazi mgahawani kwa ujira wa 2500 kwa siku.Nikawa kila hela ninayoipata basi yote namuachia mke wangu.
Nakumbuka kuna siku nilikuwa nakaanga maandazi,ila kwa bahati mbaya moto ulikuwa mkali,kwahiyo maandazi yalibabuka badala ya kuiva.Bosi alipokuja akanifukuza na kunipora simu ndogo ya batani kwa madai kwamba anafidia unga niliouchezea.
Nilitafuta mgahawa mwingine nikawa nafanya kazi ila nao nilifukuzwa kwa kosa la kubishana na Boss.
Mke wangu muda wote yupo tu ametulia nyumbani na ujauzito wake ambao sasa ulishatimiza miezi sita.
Kodi ya nyumba nadaiwa,bili ya umeme nadaiwa,chakula ndani hakuna na kazi sina,nitafanyaje?.Nilichanganyikiwa sana ila nashukuru mungu baada ya siku chache nikapata kazi ya kubeba zege.
Ikanibidi nianze kazi ya kubeba zege katika ujenzi wa kiwanda cha alizeti cha 'Pyxus agriculture' kilichopo mtaa wa viwandani maeneo ya 'Four ways'.
Asikwambie mtu,mziki wa zege ni zaidi ya rege.Ndoo ndogo tu ya lita kumi iliyojazwa tope la simenti,mchanga na kokoto inaweza kukuliza,sembuse ndoo kubwa?.Ila hakuna namna,nilijikaza na jioni nilipokea ujira wangu wa elfu 10.Ila kwa kuwa asubuhi na mchana nilikopa chakula kwa mama lishe,basi nyumbani nikarudi na 7500.Nilifanya kazi kwa takribani mwezi mzima.Nilivumilia matusi kutoka fundi mkuu kwa kuwa nilijua kilichonileta pale.nikapata hela ya kodi na chakula.
Huku nikiwa naendelea na kazi nilijitahidi kuwatafuta wazazi wa mke wangu,nashukuru walianza kunielewa na nikawaomba wamruhusu mke wangu arudi kwao ili akajifungulie huko,walikubali.
Niliendelea na kazi ya kubeba zege hatimae nikapata nauli,nikampa mke wangu nae bila hiyana alijiandaa na siku ya tatu akasafiri kwenda kwao.
Niliachana na kazi ya kubeba zege maana ilikuwa inanifanya nilale kama maiti kutokana na maumivu na uchovu.
Nikarudia tena kazi yangu ya mgahawa.Sasa nikawa nakaanga chipsi kwa ujira wa elfu tano kwa siku.Kila nilichopata nikawa naweka akiba.Nilifanya kazi hii kwa mda mrefu.
Kuna siku mke wangu alinishauri kuwa nimfate kijijini kwao nikafanye biashara ya kununua na kuuza mazao.Kwa kuwa akiba nilikuwa nayo nilikubaliana na mawazo yake.
Kwa sasa nipo kanda ya ziwa,najishughulisha na biashara ya kununua mazao vijijini kama mpunga,karanga na dengu na kuuzia mjini.Maisha yanaenda safi ingawa bado hatujaajiriwa.Mke wangu alijifungua salama mtoto wa kike,tunaishi pamoja na tunayafurahia maisha.
Jamani biashara ya mazao inalipa,vyeti vyangu sahizi vina vumbi kabatini.
Vijana tusing'ang'anie kukaa mjini,njooni kijijini tule mema ya nchi.Kuna fursa nyingi.
JIFUNZE:
1)Mkombozi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.
2)Wasomi tusibague kazi.
3)Uvumilivu unalipa.
4)Fanya kazi kwa bidii na mpende ulienae,usimkimbie kwenye shida.
AHSANTENI.
BONYEZA ALAMA '^' HAPA CHINI KUNIPIGIA KURA.
Naomba kura yako tafadhali.

Upvote
25