Michael Dudicoff
JF-Expert Member
- Aug 20, 2024
- 233
- 296
Chanzo . BBC Swahili.
Mahakama nchini Zambia imewahukumu wanaume wawili kifungo cha miaka miwili jela kwa kujaribu kutumia uchawi kumuua Rais Hakainde Hichilema.
Mzambia Leonard Phiri na Msumbiji Jasten Mabulesse Candunde walitiwa hatiani chini ya Sheria ya Uchawi baada ya kukamatwa mwezi Disemba wakiwa na hirizi, akiwemo kinyonga hai.
"Ni maoni yangu kwamba wafungwa hawakuwa tu adui wa mkuu wa nchi lakini pia walikuwa maadui wa Wazambia wote," hakimu Fine Mayambu alisema katika uamuzi wake.
Kesi hiyo imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu nchini Zambia, kwani hii ilikuwa mara ya kwanza kwa mtu yeyote kufikishwa mahakamani kwa kujaribu kutumia uchawi dhidi ya rais.
Upande wa mashtaka ulidai kuwa Phiri na Candunde walikodiwa na aliyekuwa mbunge mtoro ili kumroga Hichilema.
Licha ya kusisitiza kuwa walikuwa waganga wa jadi, mahakama iliwakuta na hatia katika makosa mawili chini ya Sheria ya Uchawi.
"Wawili hao walikubali umiliki wa hirizi hizo. Phiri alionyesha zaidi kwamba mkia wa kinyonga, ambao mara moja ungechomwa na kutumiwa katika tambiko, ungesababisha kifo kutokea ndani ya siku tano," Hakimu Mayambu alisema.
Wakili wa watu hao wawili, Agrippa Malando, alisema wateja wake waliomba kuhurumiwa kwa kuwa walikuwa wakosaji kwa mara ya kwanza.
Aliitaka mahakama kuwatoza faini, lakini ombi hilo lilikataliwa.
Hakimu Mayambu alibainisha kuwa watu wengi nchini Zambia, kama katika nchi nyingine za Afrika, waliamini uchawi, ingawa haukuthibitishwa kisayansi.
Sheria hiyo iliundwa ili kulinda jamii dhidi ya hofu na madhara yanayosababishwa na wale wanaodai kuwa na uwezo wa kufanya vitendo vya uchawi, alisema.
"Swali si kama washtakiwa ni wachawi au wana nguvu zisizo za kawaida. Ni kwamba wao wenye walionyesha kuwa ni wachawi, na ushahidi unaonyesha wazi kuwa walifanya hivyo," Hakimu Mayambu alisema.
Mbali na kifungo cha miaka miwili walichopewa kwa kosa la "kukiri" uchawi, watu hao walihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kukutwa na hirizi.
Kwa kuwa hukumu hizo zitaendeshwa kwa wakati mmoja, watatumikia kifungo cha miaka miwili pekee, kuanzia tarehe ya kukamatwa kwao Desemba 2024.
Hichilema amewahi kusema haamini katika uchawi. Hajazungumzia kesi hiyo.
Wakili Dickson Jere aliambia BBC kwamba Sheria ya Uchawi ilipitishwa wakati wa utawala wa kikoloni mwaka wa 1914.
Alisema watu "ni mara chache sana" kufunguliwa mashtaka kwa kufanya uchawi, lakini ilisaidia kuwalinda vikongwe na makundi mengine dhidi ya kutuhumiwa za kuroga au kusababisha kifo.
Uchawi pia umejitokeza sana katika mazungumzo kuhusu mzozo wa muda mrefu kati ya serikali na familia ya marehemu Rais Edgar Lungu kuhusu mazishi yake.
Baadhi ya watu wanaamini kwamba msisitizo wa serikali kwamba azikwe Zambia, kinyume na matakwa ya familia yake, unaweza kuwa ni kwa "sababu za uchawi".
Serikali imekanusha tuhuma hizo.
Lungu alifariki dunia nchini Afrika Kusini mwezi Juni, na mwili wake bado upo katika chumba cha kuhifadhia maiti huko kwa sababu ya kushindwa kufikia muafaka juu ya maziko yake.