16 September 2025
Lusaka, Zambia
Watu wailu wafungwa kwa kupanga njama ya kumuua rais wa Zambia kwa lutumia uchawi
12:45 jioni
Rais wa, Zambian Hakainde Hichilema akisikiliza mada tunduizi closing katika mkutano Mpango Mpya Wa Kifedha Duniani
Jaji mmoja nchini Zambia amewahukumu watu wawili wanaume kifungo cha miaka miwili jela na kazi ngumu baada ya kukutwa na hatia ya kupanga kumuua rais kwa kutumia uchawi.
Wanaume hao, raia wa Zambia na raia wa Msumbiji, walitiwa hatiani chini ya sheria ya uchawi ya enzi za ukoloni wiki iliyopita.
Mahakama iligundua kuwa walikuwa na hirizi, akiwemo kinyonga aliye hai, mkia wa mnyama na chupa 12 za michanganyiko hiyo na walikuwa na nia ya kuzitumia kumroga Rais Hakainde Hichilema kwa nia ya kumuua.
Leonard Phiri, 43, na Jasten Candunde, 42, waliomba msamaha kutoka kwa hakimu aliyewahukumu.
Sheria ya uchawi ya Zambia, iliyopitishwa mwaka wa 1914, inafafanua kufanya uchawi kuwa n kutumia aina yoyote ya nguvu zisizo za kawaida, ulozi, au ulozi unaokusudiwa kusababisha woga, kuudhika, au kuumia. Hukumu ya juu zaidi ni kifungo cha miaka mitatu jela