Wawili wafikishwa Mahakamani kwa ubakaji mwanafunzi

Wawili wafikishwa Mahakamani kwa ubakaji mwanafunzi

mwanausangi

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2021
Posts
548
Reaction score
608
Wanaume wawili wakazi wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kubaka na kulawiti mwanafunzi wa darasa la nne na wa kidato cha pili.

Washtakiwa hao Mathias Mkokoteni (43), mkazi wa Kata ya Mpwapwa Mjini, Mtaa wa Igovu, anadaiwa kubaka na kulawiti mtoto wa miaka 13, anayesoma shule ya msingi Igovu kati ya mwezi Juni na Julai, huku mshtakiwa Christian Mgongo (18), anadaiwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Berege mwenye umri wa miaka 14.

Kesi hizo zinasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mpwapwa, Nurupudesia Nasaary.

Akimsomea Shitaka lake, Mwendesha Mashtaka wa Polisi Joseph Michael, alidai mahakamani kuwa, Mkokoteni, alifanya tukio hilo katika Mtaa wa Igovu, Kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa, ambapo alimbaka na kumlawiti binti mwenye umri wa miaka 13.

Kwa upande wake Mgongo, ilidaiwa alifanya tukio hilo katika Kijiji cha Berege, Wilaya ya Mpwapwa, Septemba 24, mwaka huu kwa kumbaka mwanafunzi wa kidato cha pili wa Shule ya Sekondari ya Mazae.

credit: Millard Ayo
 
Tunahitaji utafiti ya nini kinaendelea kwenye bongo za watu hii nchi. Hizi kesi zimekithiri mno. Watu wanaishia kusema Mungu asaidie watoto wetu badala ya kuchukua hatua!
 
jumatatatu nimepiga 3, jumanne nimepiga 2 jumatano nimepumzika .leo alhamisi nimepiga 2 Safi kabisa no stress,hakuna baby nauli,baby sijala
 

Wababa tuache kupenda watoto, huyu wa miaka 43 unakuta hako huyo mtoto wa miaka 13 alikuwa mpenzi wake.

Wazazi pia tujitahidi sana kuwafundisha watoto wetu kuridhika na wanavyopata nyumbani. Wakati huohuo tujitahidi kuwatimizia watoto wetu mahitaji yao ya muhimu.

Mara nyingi hawa watoto wanadanganywa na vitu vidogo sana na vya aibu, lakini unakuta kweli mzazi yupo na havitimizi.
 
Kuna ulazima kwa wazazi kuanzisha ulinzi shirikishi dhidi ya watoto wetu. Maana hali kwa sasa ni mbaya.
 
Umasikini ndo chanzo kikuu Cha haha you're katika nchi nyingi za kiAfrica.

Idle minds are devil's workshop.
 
Back
Top Bottom