Wawili wakamatwa kwa kuhusika na shamulio la ugaidi

Wawili wakamatwa kwa kuhusika na shamulio la ugaidi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Maafisa wa polisi jijini Nairobi wamewakamata washukiwa wawili wanaoaminika walihusika pakubwa katika kupanga shambulizi la kigaidi katika hoteli ya kifahari ya DustiD2 eneo la 14 Riverside.

Mwanamke aliyetambulika kwa jina moja kama Kemunto, alipatikana ndani ya nyumba ya mshukiwa mmoja wa ugaidi mtaani Ruaka.

Kama ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, wapiganaji wa al -Shabaab walikiri kutekeleza shambulizi hilo Jumanne, Januari 15 ambapo watu 21 waliripotiwa kupoteza maisha yao huku wengi wakiachwa na majeraha mabaya ya risasi.

Mkurugenzi mkuu wa upelelezi, DCI George Kinoti alithibitisha kwamba mshukiwa wa kike alikamatwa akiwa mtaa wa Mucatha, Ruaka huku mshukiwa mwingine wa kiume akikamatwa akiwa mtaani Easyleigh.

" Wawili hao wanatupatia taarifa muhimu kuhusiana na shambulio la 14 Riverside, tumefanya uchunguzi na tumebaini kwamba walikuwa wakiwasiliana sana na magaidi ambao waliuwawa na polisi. Bado tunawasaka washukiwa zaidi ambao walichangia katika kupanga shambulio hilo," Kinoti alisema.

Kinoti alisema washukiwa hao wawili walikuwa wakiwasiliana moja kwa moja na magaidi hao waliouwawa na maafisa wa polisi kwenye shambulizi hilo.

Awali, maafisa wa upelelezi waliofika nyumbani kwa mmoja wa magaidi walisema walipata vifaa vinavyotumika kutengeneza vilipuzi na silaha zingine hatari ikiwemo bunduki kadhaa za AK47 zinazosemekana kutoka Somalia.
 
Back
Top Bottom