Waya hauwezi kutoka NIDA kwenda bank accounts za CCM na sisi tupate ya soda?

Waya hauwezi kutoka NIDA kwenda bank accounts za CCM na sisi tupate ya soda?

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Ni dhahiri sasa huu uchaguzi sio tena kwa ajili ya kuchagua wawakilishi wa wananchi. Ni dhahiri sasa hawa CCM hawapo tena kuhakikisha ustawi wa Tanzania. Wewe umeona wapi mtu anatumia gharama kubwa na mbinu za aibu eti kwa ajili ya kutaka kukuwakilisha?
Huu ni uchaguzi kwa ajili awamu nyingine ya kula mema ya nchi. Mwananchi anaenda kuliwa vizuri.

Kwa hali hiyo, tuwaombe wahusika waliounga waya kutoka NEC kwenda NIDA, waunganishe huo waya kwenye miamala ya fedha za CCM. Vyovyote mtakavyofanya hakikisheni mnapotumia NIDA zetu na sisi tulipwe chochote. Huko NIDA kuna namba zetu za simu, tutumieni kiongeza ujinga tuzidi kunyamaza mfanye yenu.
 
Ni dhahiri sasa huu uchaguzi sio tena kwa ajili ya kuchagua wawakilishi wa wananchi. Ni dhahiri sasa hawa CCM hawapo tena kuhakikisha ustawi wa Tanzania. Wewe umeona wapi mtu anatumia gharama kubwa na mbinu za aibu eti kwa ajili ya kutaka kukuwakilisha?
Huu ni uchaguzi kwa ajili awamu nyingine ya kula mema ya nchi. Mwananchi anaenda kuliwa vizuri.

Tena wamejipangia kabisa na wabunge wao ili wale kwa utulivu. Yaani wananchi hawawezi kuteua wawakilishi wao wenyewe?

Aibu sana, yaani hata walioteuliwa na kupitishwa kwa kura nyingi na wananchi bado wanaenguliwa kwa mapenzi/matakwa ya mtu mmoja?

Kwa nini wasiache wananchi waamue ili kudhihirisha na kuheshimu dhana ya kwamba mamlaka hutoka kwa wananchi?

Njia ya mwongo ni fupi, yote yana mwisho.
 
Back
Top Bottom