Waya: Ngoma mpya ya Joh Makini mbaya kuliko zote toka kwake

WEWE HUJUI MUZIKI HIVI UNAJUA WIMBO ULIOMPA UMAARUFU JOH MAKINI? NA UMETENGENEZWA NA NANI?
 
PRODUCERS WALIOKUWA WANAJUA KUMPATIA JOH MAKINI
1. MANDUGU DIGITAL BY DUNGA
2.KAMA KAWA RECORD BY YUDDI
3.BHITS BY PANCHO LATINO
4. PRODUCER Q THE DON
5. NAH REAL
 
JOH MAKINI NA WEUSI WAMEMKIMBIA NAH REAL KWAKUWA WALIKUWA WANAPENDA MTEREMKO KULIPA HELA YA STUDIO ILIKUWA NGUMU KWAO LICHA YAKUWA NA MAJINA MAKUBWA SASA LAANA IMEANZA KUWAPATA
 
Acha uchawi were nyimbo mbona nzuri tu na itafanya vizuri, John making amejaribu radha nyingine music tofauti na tulivyomzoea
Ni kitu kizuri
Hata davido alijaribu ladha tofauti alivyoona mambo kombo kaamua kurudi alipotoka
 
WEWE HUJUI MUZIKI HIVI UNAJUA WIMBO ULIOMPA UMAARUFU JOH MAKINI? NA UMETENGENEZWA NA NANI?
Namfahamu Joh Makini tangu album ya Zamu yangu enzi hizo ulikuwa unanyonya.Wimbo uliompa umaarufu Joh Makini ni HAO wakati unatoka wewe na Nahreel mlikuwa bado mnanyonya.

Joh hajawahi kutoa nyimbo kali zaidi ya hio.Kuanzia lyrics,flow,beat even video kwa wakati ule ilikuwa poa
 
BASI HUJUI MUZIKI BORA UKAE KIMYA,WIMBO ULIOMUWEKA KWENYE RAMANI YA MUZIKI MPAKA AKAWA GUMZO NI STIMU ZIMELIPIWA
 
Huyu ndiyo alikuwa the real rapture [emoji41] [emoji41]

Hii ngoma kila nikiisikiliza huwa najiuliza hivi kuna siku atakuja kutoa mfanano wa ngoma kama hii?

Hii ngoma ilikuwa blessed
 
JOH MAKINI NA WEUSI WAMEMKIMBIA NAH REAL KWAKUWA WALIKUWA WANAPENDA MTEREMKO KULIPA HELA YA STUDIO ILIKUWA NGUMU KWAO LICHA YAKUWA NA MAJINA MAKUBWA SASA LAANA IMEANZA KUWAPATA
Mkuu naona umekoma na weusi kumkimbia nahreal toka jana kwa hiyo ulitaka maisha yote ya mziki wayamalizie kwa nahreal?
 
Mkiweka ushabiki pembeni na mapenzi binafsi kwa mwamba was kaskazi, ukajaribu kujivua mapenzi yako kwake na kuangalia ubora wa kazi zake za muziki, wimbo huu no WABARIDI SANA, achana na uandishi na flow anza kujudge bits za wimbo na pitch zake huu ni wimbo MBOVU KABISA kuwahi kufanywa na nguli huyu wa bongo lava/hip hop. Ila kwa kuwa no "mwana wetu" wimbo huu tutawalazimisha muupende tu! tutaupiga sana katika radio yetu pendwa na promo za pale na hapa mpaka mtaupenda tu ingawa kiuhalisia ni wimbo BUTU Umefubaa!...levo ya wimbo huu ulipaswa kutolewa na kina luteni kalama na mwenzie sio kwa watu was levo za Mwamba au Ngosha Ze Don FidQ mwana aliye juu!
 
mimi sio mpnz wa hip hop ila huu uwimbo nimeupenda saaana tena sana
 
Unataka kuniambia wapenzi wa music ni mbumbumbu na mapoyoyo wanalazimishwa kupenda wimbo mbovu? Zama hivi kuna radio na TV chungu nzima? Ukiona kitu kibaya unauwezo wa kubadilisha Chanel?
Inaitaji akili za kihayawani kuamini watu na akili zao timamu wanalazimishwa kupenda nyimbo mbovu na wanatoa pesa kwenda kwenye matamasha kuburudika na hizo nyimbo mbovu.
 
Watanzania bhana!! Kisa flani amesema anabebwa basi na wao akili zao zimeelekea huko huko, zamani walikuwa wapi sijui kulijua hilo. Hawatumii akili zao ila wanajudge kwa akili na maoni ya wengine.
 
1.Stimu Zimelipiwa
2.Ufalme
3.Chochote Popote

Bonus Track
-Muda
-Manuva
-Zamu Yangu.

Hizi ndio ngoma zangu kali za Muda wote toka kwa Mwamba
 
Nyimbo mbaya tu. Wanatumia hela nyingi kushoot video.

Ukiuliza atakwambia katumia milion 20. Wakati kwa wimbo huo alistahiri kutumia milioni mbili.
 
Hakuna kitu apo nyimbo mbovu iyo ila kwakua ni Joh makini itapata promo ila honestly...hamna kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…