Wayahudi wana muono bora zaidi kuhusu shetani kuliko wakristo

Wayahudi wana muono bora zaidi kuhusu shetani kuliko wakristo

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Sikiliza tu huu utitiri wa redio za wakristo usikie vituko kama si vichekesho. Shetani na mapepo yanaogopwa na kutajwa mara nyingi kuliko Mungu.

Wanabwabwaja usiku na mchana mpaka sauti zao zimeharibika. Wewe pepo, wewe jini, achia ,achia, kwa jina la Yesu!

Hao Wayahudi ambao wakristo wanawalaumu kwa kumkataa Yesu, ambao ndio wao Mungu alinena nao kwanza hawana upumbavu huu.

Wanamuelewa shetani ni nani. Wakristo kwa hilo wamefeli kabisa. Shetani wanamuona kila mahali kuliko wanavyomuona Mungu. Tuondoleeni hii aibu.

Mnajidhalilisha mbele ya kiumbe ambacho Mungu akisema zimika kinazimika. Imani yenu iko wapi?

Shetani ni malaika na hawezi kufanya jambo isipokuwa kwa ridhaa ya Mungu. Kumbukeni hadithi ya Ayubu.
 
Sikiliza tu huu utitiri wa redio za wakristo usikie vituko kama si vichekesho. Shetani na mapepo yanaogopwa na kutajwa mara nyingi kuliko Mungu. Wanabwabwaja usiku na mchana mpaka sauti zao zimeharibika. Wewe pepo, wewe jini, achia ,achia, kwa jina la Yesu! Hao Wayahudi ambao wakristo wanawalaumu kwa kumkataa Yesu, ambao ndio wao Mungu alinena nao kwanza hawana upumbavu huu. Wanamuelewa shetani ni nani. Wakristo kwa hilo wamefeli kabisa. Shetani wanamuona kila mahali kuliko wanavyomuona Mungu. Tuondoleeni hii aibu. Mnajidhalilisha mbele ya kiumbe ambacho Mungu akisema zimika kinazimika. Imani yenu iko wapi? Shetani ni malaika na hawezi kufanya jambo isipokuwa kwa ridhaa ya Mungu. Kumbukeni hadithi ya Ayubu.
Kwa hiyo wafanyeje?Wasikemee pepo!
 
Ubarikiwe, umenena hakika. Dini zinahubiri shetani badala ya Mungu.
 
Kwa hiyo wafanyeje?Wasikemee pepo!
Wakemee mara moja tu kwa jina la Yesu. Kama mara moja haitoshi mtu anarudia mara 20 huyo ni Yesu mwingine. Maana Yesu wa uongo wapo pia. Ukikemea mara moja hatoki hapo ni wazi wewe Yesu wako ni wa bandia. Soma hata kitabu cha matendo ya mitume. Mitume hawakufanya huu upumbavu wa hawa wahubiri miujiza feki.
 
Hekedeedeee hikabaaa kwa jina la Yesu shatakabaya kwa jina la Yesu nakemea hikatakabaya. Ayamatakayaayaaya shatakabaya........
..!!! Iko redio moja Arusha zaidi ya nusu saa iko hewani anakemea mapepo na sijui atamaliza saa ngapi!!
 
Ukienda Tunduma na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya unaweza usilale kabisa usiku kwa hizo kelele za walokole. Kimsingi walokole ni washirikina ndo maana mahubiri yao mengi ni kuhusu uchawi.
 
Na jumapili ijayo wanaenda tena kumlaani shetani waliemlaani wiki iliyopita
 
Leo Trump alikuwa nadhani Capitol nilisikiliza hotuba yake alfajiri akisema wanaaanga wa marekani wataenda kuweka bendera ya Marekani kwenye sayari ya Mars na mbali zaidi (and beyond). Hao ndio wale Mungu aliwapa talanta wanazitumia vema. Sisi talanta tumefukia chini tunakesha kuomba miujiza na kukemea mapepo. Tutapata adhabu iliyo kuu, Yesu mwenyewe alisema!
 
Ukienda Tunduma na baadhi ya maeneo ya mkoa wa Mbeya unaweza usilale kabisa usiku kwa hizo kelele za walokole. Kimsingi walokole ni washirikina ndo maana mahubiri yao mengi ni kuhusu uchawi.
Sioni tofauti yoyote kati yao na wale wanamazingaombwe walikuwa wakiongea lugha zisizoeleweka sijui kababayeee! Tukio la siku ya pentecostal na mafundisho ya Mtume Paulo ama hawakuyaelewa au wamepotosha kwa makusudi.
 
Na jumapili ijayo wanaenda tena kumlaani shetani waliemlaani wiki iliyopita
Watapewa kichwa cha somo kingine. Kama wiki iliyopita waliambiwa LEO NI SIKU YA KUVUNJA MADHABAHU ZOTE ZINAZOKUTESA wiki ijayo wataambiwa ZLEO NI SIKU YA KUFUNGULIWA MILANGO YA KIFEDHA. Wiki nyingine wataambiwa LEO NI SIKU YA KUFUNGUA MALANGO YA MZALIWA WA KWANZA. Kila siku kuna neno la kuwapumbaza watu. Maneno hayaishi. Kwenye hesabu kuna kitu kinaitwa combinatorics. Chukua namba kadhaa halafu uzipange katika mipangilio tofauti isiyofanana uone kwa mfano chukka namba moja mpaka saba uzichanganyechanganye uone utapata namba ngapi tofauti. Ni maelfu kwa maelfu. Ndio hawa wahubiri. Kila siku wana mada tofauti ili ubaki kanisani kwake akutafune vizuri!
 
Sikiliza tu huu utitiri wa redio za wakristo usikie vituko kama si vichekesho. Shetani na mapepo yanaogopwa na kutajwa mara nyingi kuliko Mungu. Wanabwabwaja usiku na mchana mpaka sauti zao zimeharibika. Wewe pepo, wewe jini, achia ,achia, kwa jina la Yesu! Hao Wayahudi ambao wakristo wanawalaumu kwa kumkataa Yesu, ambao ndio wao Mungu alinena nao kwanza hawana upumbavu huu. Wanamuelewa shetani ni nani. Wakristo kwa hilo wamefeli kabisa. Shetani wanamuona kila mahali kuliko wanavyomuona Mungu. Tuondoleeni hii aibu. Mnajidhalilisha mbele ya kiumbe ambacho Mungu akisema zimika kinazimika. Imani yenu iko wapi? Shetani ni malaika na hawezi kufanya jambo isipokuwa kwa ridhaa ya Mungu. Kumbukeni hadithi ya Ayubu.
Hizo redio za Wayahudi umezisikilizia wapi wakati hata passport hauna?
 
Toka shetani, kumbuka shetani ni roho, ana uwezo mkubwa kuliko binadamu. Unamkemeaje? Ni vituko! Badala ya kumuomba Mungu amuondoe shetani katika uso wa dunia unamkemea. Siku akiwageuka mtakauka wote, anawaona kama vitoto vinavyocheza.
 
Back
Top Bottom